Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Biblia Kwenye Mtandao | BIBLIA TAKATIFU—TAFSIRI YA ULIMWENGU MPYA (TOLEO LA 2017)

Ayubu 13:1-28

MUHTASARI WA YALIYOMO

  • Ayubu aendelea kujibu (1-28)

    • ‘Ni afadhali nizungumze na Mungu’ (3)

    • ‘Ninyi ni matabibu wasiofaa kitu’ (4)

    • “Najua sina kosa” (18)

    • Auliza kwa nini Mungu anamwona kuwa adui (24)

13  “Naam, jicho langu limeona hayo yote,Sikio langu limesikia na kuyaelewa.   Mnayojua, mimi pia nayajua;Mimi si duni kwenu.   Lakini mimi, ni afadhali nizungumze na Mweza-Yote mwenyewe;Ninatamani kujitetea mbele za Mungu.+   Lakini ninyi mnanipaka uwongo;Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa kitu.+   Laiti mngenyamaza kabisa,Mngeonekana kuwa wenye hekima.+   Tafadhali, sikilizeni hoja zangu,Na msikilize ninapojitetea kwa midomo yangu.   Je, mtasema mambo yasiyo ya haki kwa niaba ya Mungu,Na je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa ajili yake?   Je, mtamuunga mkono,*Je, mtajaribu kumtetea Mungu wa kweli?   Je, mambo yatawaendea vyema akiwachunguza?+ Je, mtamdanganya kama mnavyomdanganya mwanadamu anayeweza kufa? 10  Kwa hakika atawakemeaMkijaribu kwa siri kuonyesha upendeleo.+ 11  Je, adhama yake mwenyewe haitawaogopeshaNa hofu yake haitawaangukia? 12  Misemo yenu ya hekima* ni methali za majivu;Kujitetea kwenu* ni hafifu kama ngome za udongo. 13  Nyamazeni mbele yangu, ili niongee. Kisha na yanipate yatakayonipata! 14  Kwa nini ninajihatarisha*Na kubeba uhai wangu* mikononi mwangu? 15  Hata akiniua, bado nitangoja;+Nitajitetea* mbele zake. 16  Ndipo atakapokuwa wokovu wangu,+Kwa maana hakuna mtu aliyemkataa Mungu* anayeweza kuja mbele zake.+ 17  Sikilizeni kwa makini neno langu;Sikilizeni tangazo langu. 18  Sasa tazameni, nimetayarisha kesi yangu;Najua sina kosa. 19  Ni nani atakayepambana nami? Nitakufa, ikiwa nitanyamaza!* 20  Ee Mungu, nifanyie mambo mawili tu,*Ili nisijifiche kutoka mbele zako: 21  Ondoa mkono wako mzito uwe mbali nami,Nawe usiache hofu yangu kukuelekea initishe.+ 22  Niite nami nitakujibu,Au acha nizungumze, nawe unijibu. 23  Nimefanya makosa na dhambi gani? Nifunulie kosa langu na dhambi yangu. 24  Kwa nini unauficha uso wako+Na kuniona kuwa adui yako?+ 25  Je, utajaribu kulitisha jani linalopeperushwa na upepoAu kuyakimbiza majani makavu? 26  Kwa maana unaendelea kuandika mashtaka makali dhidi yangu,Nawe unanifanya niwajibike kwa sababu ya dhambi nilizofanya nilipokuwa kijana. 27  Umeitia miguu yangu katika mikatale,Unavichunguza kwa makini vijia vyangu vyote,Nawe unafuata kila wayo wa mguu wangu. 28  Kwa hiyo mwanadamu* huoza kama kitu kilichooza,Kama vazi lililoliwa na nondo.*

Maelezo ya Chini

Au “mtampendelea.”
Au “inayokumbukwa.”
Tnn., “Mafundo ya ngao zenu.”
Tnn., “Kwa nini naubeba mwili wangu kwenye meno yangu?”
Au “nafsi yangu.”
Au “Nitatetea njia zangu.”
Au “mwasi imani.”
Au labda, “Ikiwa mtu anaweza kupambana nami, nitanyamaza na kufa.”
Tnn., “Mambo mawili tu, usinitendee.”
Labda “mwanadamu” anayerejelewa ni Ayubu.
Aina fulani ya mdudu mharibifu.