Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Waamuzi 12:1-15

12  Ndipo watu wa Efraimu wakakusanywa pamoja na kuvuka kuelekea kaskazini, nao wakamwambia Yeftha: “Kwa nini ulivuka kupigana na wana wa Amoni, nawe hukutuita twende pamoja nawe?+ Nyumba yako tutaiteketeza juu yako kwa moto.”+  Lakini Yeftha akawaambia: “Mimi na watu wangu tulikuwa na ugomvi mkubwa pamoja na wana wa Amoni.+ Nami nikawaomba ninyi msaada, wala hamkuniokoa kutoka mkononi mwao.  Nilipoona kwamba hamniokoi, nikaazimia kuitia nafsi yangu mkononi+ mwangu mwenyewe, nikavuka kupigana na wana wa Amoni.+ Hivyo Yehova akawatia mkononi mwangu. Basi kwa nini mmekuja juu yangu kupigana nami leo?”  Basi bila kukawia Yeftha akakusanya watu wote wa Gileadi,+ akapigana na Efraimu; na watu wa Gileadi wakapiga Efraimu, kwa maana walikuwa wamesema: “Ninyi Gileadi ni watu walioponyoka kutoka Efraimu, kutoka ndani ya Efraimu, kutoka ndani ya Manase.”  Nao Gileadi wakateka vivuko vya Yordani+ mbele ya Efraimu; ndipo ikatukia kwamba wakati watu wa Efraimu waliokuwa wakikimbia waliposema: “Niache nivuke,” ndipo watu wa Gileadi wakawa wakimwambia kila mmoja wao: “Je, wewe ni Mwefraimu?” Akisema: “Hapana!”  ndipo walipomwambia: “Tafadhali sema Shibolethi.”+ Naye alisema: “Sibolethi,” kwa kuwa hakuweza kutamka neno hilo kwa usahihi. Nao walimshika na kumuua kwenye vivuko vya Yordani. Basi wakati huo wakaanguka watu 42,000 kutoka katika Efraimu.+  Na Yeftha akaendelea kuhukumu Israeli kwa miaka sita, kisha Yeftha Mgileadi akafa, akazikwa katika jiji lake kule Gileadi.  Naye Ibzani kutoka Bethlehemu+ akaanza kuhukumu Israeli baada yake.+  Naye akawa na wana 30 na binti 30. Akatuma watu nje kuleta binti 30 kwa ajili ya wanawe kutoka nje. Naye akaendelea kuhukumu Israeli kwa miaka saba. 10  Kisha Ibzani akafa, akazikwa Bethlehemu. 11  Na baada yake Eloni Mzabuloni+ akaanza kuhukumu Israeli. Naye akaendelea kuhukumu Israeli kwa miaka kumi. 12  Kisha Eloni Mzabuloni akafa, akazikwa Aiyaloni katika nchi ya Zabuloni. 13  Na baada yake Abdoni mwana wa Hileli Mpirathoni+ akaanza kuhukumu Israeli. 14  Naye akaja kuwa na wana 40 na wajukuu 30 waliopanda punda wakomavu+ 70. Naye akaendelea kuhukumu Israeli kwa miaka minane. 15  Kisha Abdoni mwana wa Hileli Mpirathoni akafa, akazikwa Pirathoni katika nchi ya Efraimu katika mlima wa Mwamaleki.+

Maelezo ya Chini