Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Hesabu 33:1-56

33  Hivi ndivyo vilivyokuwa vituo vya wana wa Israeli waliotoka nchi ya Misri+ kwa majeshi+ yao kwa mkono wa Musa na Haruni.+  Naye Musa akaendelea kuandika mahali walipoondoka, kulingana na vituo vyao kwa agizo la Yehova; navyo hivi ndivyo vilivyokuwa vituo vyao kutoka mahali pamoja walipoondoka mpaka pengine:+  Nao wakaondoka Ramesesi+ katika mwezi wa kwanza, katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza.+ Siku ileile iliyofuata pasaka+ wana wa Israeli wakatoka kwa mkono ulioinuliwa mbele ya macho ya Wamisri wote.+  Wakati wote huo, Wamisri walikuwa wakiwazika wale ambao Yehova alikuwa amewapiga katikati yao, yaani, wazaliwa wote wa kwanza;+ na juu ya miungu yao Yehova alikuwa amefanya hukumu.+  Kwa hiyo wana wa Israeli wakaondoka Ramesesi,+ wakapiga kambi Sukothi.+  Kisha wakaondoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu,+ ambapo pako ukingoni mwa nyika.  Halafu wakaondoka Ethamu, wakageuka na kurudi nyuma kuelekea Pihahirothi,+ ambapo panaelekeana na Baal-sefoni;+ nao wakapiga kambi mbele ya Migdoli.+  Halafu wakaondoka Pihahirothi, wakapita katikati ya bahari+ mpaka nyikani,+ wakaendelea kupiga mwendo safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu,+ wakapiga kambi Mara.+  Kisha wakaondoka Mara wakaja Elimu.+ Sasa katika Elimu kulikuwa na mabubujiko 12 ya maji na mitende 70. Kwa hiyo wakapiga kambi huko. 10  Kisha wakaondoka Elimu, wakapiga kambi kando ya Bahari Nyekundu. 11  Baada ya hapo wakaondoka katika Bahari Nyekundu, wakapiga kambi katika nyika ya Sini.+ 12  Halafu wakaondoka katika nyika ya Sini, wakapiga kambi Dofka. 13  Baadaye wakaondoka Dofka, wakapiga kambi Alushi. 14  Kisha wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu.+ Na huko kukawa hakuna maji ya kunywa kwa ajili ya watu. 15  Baada ya hapo wakaondoka Refidimu, wakapiga kambi katika nyika ya Sinai.+ 16  Halafu wakaondoka katika nyika ya Sinai, wakapiga kambi Kibroth-hataava.+ 17  Kisha wakaondoka Kibroth-hataava, wakapiga kambi Haserothi.+ 18  Baada ya hapo wakaondoka Haserothi, wakapiga kambi Rithma. 19  Kisha wakaondoka Rithma, wakapiga kambi Rimon-peresi. 20  Halafu wakaondoka Rimon-peresi, wakapiga kambi Libna. 21  Baadaye wakaondoka Libna, wakapiga kambi Risa. 22  Kisha wakaondoka Risa, wakapiga kambi Kehelatha. 23  Halafu wakaondoka Kehelatha, wakapiga kambi katika Mlima Sheferi. 24  Baada ya hapo wakaondoka Mlima Sheferi, wakapiga kambi+ Harada. 25  Halafu wakaondoka Harada, wakapiga kambi Makelothi. 26  Kisha wakaondoka+ Makelothi, wakapiga kambi Tahathi. 27  Baada ya hapo wakaondoka Tahathi, wakapiga kambi Tera. 28  Halafu wakaondoka Tera, wakapiga kambi Mithka. 29  Baadaye wakaondoka Mithka, wakapiga kambi Hashmona. 30  Kisha wakaondoka Hashmona, wakapiga kambi Moserothi. 31  Halafu wakaondoka Moserothi, wakapiga kambi Bene-yaakani.+ 32  Baada ya hapo wakaondoka Bene-yaakani, wakapiga kambi Hor-hagidgadi. 33  Kisha wakaondoka Hor-hagidgadi, wakapiga kambi Yotbata.+ 34  Baadaye wakaondoka Yotbata, wakapiga kambi Abrona. 35  Halafu wakaondoka Abrona, wakapiga kambi Esion-geberi.+ 36  Baada ya hapo wakaondoka Esion-geberi, wakapiga kambi katika nyika ya Zini,+ yaani, Kadeshi. 37  Baadaye wakaondoka Kadeshi, wakapiga kambi katika Mlima Hori,+ kwenye mpaka wa nchi ya Edomu. 38  Naye Haruni kuhani akapanda katika Mlima Hori kwa agizo la Yehova, akafa huko katika mwaka wa 40 tangu wana wa Israeli walipotoka katika nchi ya Misri, katika mwezi wa 5, siku ya kwanza ya mwezi huo.+ 39  Naye Haruni alikuwa na umri wa miaka 123 alipokufa kwenye Mlima Hori. 40  Sasa yule Mkanaani, mfalme wa Aradi,+ alipokuwa akikaa katika Negebu,+ katika nchi ya Kanaani, akapata kusikia juu ya kuja kwa wana wa Israeli. 41  Baada ya muda wakaondoka katika Mlima Hori,+ wakapiga kambi Salmona. 42  Baada ya hapo wakaondoka Salmona, wakapiga kambi Punoni. 43  Kisha wakaondoka Punoni, wakapiga kambi Obothi.+ 44  Halafu wakaondoka Obothi, wakapiga kambi Iye-abarimu kwenye mpaka wa Moabu.+ 45  Baadaye wakaondoka Iyimu, wakapiga kambi Dibon-gadi.+ 46  Baada ya hapo wakaondoka Dibon-gadi, wakapiga kambi Almon-diblathaimu. 47  Halafu wakaondoka Almon-diblathaimu,+ wakapiga kambi katika milima ya Abarimu+ mbele ya Nebo.+ 48  Mwishowe wakaondoka katika milima ya Abarimu, wakapiga kambi katika nchi tambarare za jangwa la Moabu+ kando ya Yordani, kule Yeriko. 49  Nao wakaendelea kukaa katika kambi kando ya Yordani kutoka Beth-yeshimothi+ mpaka Abel-shitimu+ katika nchi tambarare za jangwa la Moabu. 50  Na Yehova akasema na Musa katika nchi tambarare za jangwa la Moabu kando ya Yordani, kule Yeriko,+ na kumwambia: 51  “Sema na wana wa Israeli, nawe utawaambia, ‘Mtavuka Yordani kuingia katika nchi ya Kanaani.+ 52  Nanyi mnapaswa kuwafukuzia mbali wakaaji wote wa nchi hiyo kutoka mbele yenu na kuharibu maumbo yao yote ya mawe,+ nanyi mnapaswa kuziharibu sanamu zao zote za madini ya kuyeyusha,+ na mnapaswa kupaharibu mahali pao pote patakatifu.+ 53  Nanyi mtaimiliki nchi na kukaa humo, kwa sababu hakika nitawapa ninyi nchi hiyo mpate kuimiliki.+ 54  Nanyi mtaigawa nchi hiyo kwa ajili yenu iwe miliki kwa kura+ kulingana na familia zenu.+ Kwake aliye na hesabu kubwa mtaongeza urithi wake, na kwake aliye mchache mtaupunguza urithi wake.+ Mahali ambapo kura itamtokea, hapo patakuwa pake.+ Kulingana na makabila ya baba zenu mnapaswa kumiliki nchi.+ 55  “‘Hata hivyo, ikiwa hamtawafukuzia mbali wakaaji wa nchi hiyo kutoka mbele yenu,+ basi wale mtakaoacha watakuwa kama michomo katika macho yenu na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika nchi ambamo mtakuwa mkikaa.+ 56  Na itatukia kwamba kama vile nilivyokusudia kuwatendea hao, ndivyo nitakavyowatendea ninyi.’”+

Maelezo ya Chini