Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Ezekieli 48:1-35

48  “Na haya ndiyo majina ya makabila hayo. Kutoka upande wa kaskazini, upande wa njia ya Hethloni+ hadi kuingia ndani huko Hamathi,+ Hasar-enani,+ mpaka wa Damasko kuelekea kaskazini, upande wa Hamathi; nayo itakuwa na mpaka wa mashariki na wa magharibi, Dani+ fungu moja.  Na kwenye mpaka wa Dani, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Asheri+ moja.  Na kwenye mpaka wa Asheri, kutoka mpaka wa mashariki hata kwenye mpaka wa magharibi, Naftali+ moja.  Na kwenye mpaka wa Naftali, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Manase+ moja.  Na kwenye mpaka wa Manase, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Efraimu+ moja.  Na kwenye mpaka wa Efraimu, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Rubeni+ moja.  Na kwenye mpaka wa Rubeni, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Yuda+ moja.  Na kwenye mpaka wa Yuda, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, mchango ambao ninyi mnapaswa kutoa unapaswa kuwa na upana wa mikono 25,000,+ na urefu kulingana na moja la yale mafungu kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi. Napo patakatifu patakuwa katikati yake.+  “Kwa habari ya mchango ambao mnapaswa kumtolea Yehova, urefu utakuwa mikono 25,000 na upana mikono 10,000. 10  Na kwa habari yake kutakuwako mchango mtakatifu kwa ajili ya makuhani,+ upande wa kaskazini mikono 25,000, na upande wa magharibi upana wa mikono 10,000, na upande wa mashariki upana wa mikono 10,000, na upande wa kusini urefu wa mikono 25,000. Na patakatifu pa Yehova patakuwa katikati yake.+ 11  Patakuwa kwa ajili ya makuhani, waliotakaswa kutoka kwa wana wa Sadoki,+ ambao waliutunza wajibu kunielekea mimi, ambao hawakuenda mbali wakati ambapo wana wa Israeli walienda huku na huku, kama vile Walawi walivyoenda huku na huku.+ 12  Nao watakuwa na mchango kutoka katika mchango wa hiyo nchi ukiwa kitu kitakatifu zaidi, kwenye mpaka wa Walawi.+ 13  “Na Walawi watakuwa na fungu,+ karibu kabisa na eneo la makuhani, lenye urefu wa mikono 25,000, na upana wa mikono 10,000; urefu wote ukiwa 25,000, na upana ukiwa 10,000.+ 14  Nao hawapaswi kuuza sehemu yoyote kati ya hiyo, wala mtu hapaswi kubadilishana, wala mtu hapaswi kuacha sehemu bora zaidi ya nchi itoke kwao; kwa maana hicho ni kitu kitakatifu kwa Yehova.+ 15  “Kwa habari ya ile mikono 5,000 inayobaki katika upana kandokando ya ile mikono 25,000, ni kitu najisi cha jiji,+ kiwe makao na kiwe uwanja wa malisho. Nalo jiji litakuwa katikati yake.+ 16  Na hivi ndivyo vipimo vya jiji: mpaka wa kaskazini mikono 4,500, na mpaka wa kusini 4,500, na mpaka wa mashariki 4,500, na mpaka wa magharibi 4,500. 17  Na jiji litakuwa na uwanja wa malisho,+ upande wa kaskazini mikono 250, na upande wa kusini 250, na upande wa mashariki 250, na upande wa magharibi 250. 18  “Na kitakachobaki katika urefu kitalingana kabisa na mchango mtakatifu,+ mikono 10,000 upande wa mashariki, na 10,000 upande wa magharibi; napo patalingana kabisa na mchango mtakatifu, na mazao yake yatakuwa kwa ajili ya mkate wa wale wanaotumikia jiji.+ 19  Na wale wanaotumikia jiji kutoka katika makabila yote ya Israeli watapalima.+ 20  “Mchango mzima ni mikono 25,000 urefu kwa 25,000 upana. Mtachanga sehemu iliyo mraba iwe mchango mtakatifu pamoja na miliki ya jiji. 21  “Na sehemu iliyobaki itakuwa ya mkuu,+ upande huu na upande ule wa mchango mtakatifu na wa miliki ya jiji,+ kando ya mikono 25,000 ya mchango mtakatifu kuelekea mpaka wa mashariki; na upande wa magharibi kando ya mikono 25,000 kuelekea mpaka wa magharibi.+ Kama yalivyo mafungu hayo, ndivyo itakavyokuwa kwa ajili ya mkuu. Na mchango mtakatifu na patakatifu pa ile Nyumba patakuwa katikati yake. 22  “Nayo miliki ya Walawi na miliki ya jiji, itakuwa katikati ya miliki ya mkuu. Katikati ya mpaka wa Yuda+ na mpaka wa Benyamini itakuwa ya mkuu. 23  “Nayo yale makabila mengine, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Benyamini+ fungu moja. 24  Na kando ya mpaka wa Benyamini, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Simeoni+ moja. 25  Na kando ya mpaka wa Simeoni, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Isakari+ moja. 26  Na kando ya mpaka wa Isakari, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Zabuloni+ moja. 27  Na kando ya mpaka wa Zabuloni, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, Gadi+ moja. 28  Na kando ya mpaka wa Gadi, hadi mpaka wa kusini, litakuwa kuelekea kusini; nao mpaka utakuwa kutoka Tamari+ hadi maji ya Meribath-kadeshi,+ hadi kwenye bonde la mto,+ hadi kwenye ile Bahari Kuu.+ 29  “Hii itakuwa nchi ambayo mtafanya iangukie makabila ya Israeli kwa kura iwe urithi,+ na hayo yatakuwa mafungu yao,”+ asema Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova. 30  “Na haya yatakuwa malango ya kutokea ya jiji: Kwenye mpaka wa kaskazini, kipimo kitakuwa mikono 4,500.+ 31  “Na malango ya jiji yatakuwa kulingana na makabila ya Israeli, malango matatu yakiwa upande wa kaskazini, lango la Rubeni, moja; lango la Yuda, moja; lango la Lawi, moja. 32  “Na kwenye mpaka wa mashariki kutakuwa mikono 4,500, na malango matatu, naam, lango la Yosefu, moja; lango la Benyamini, moja; lango la Dani, moja. 33  “Na mpaka wa kusini utakuwa mikono 4,500 kipimo chake, ukiwa na malango matatu, lango la Simeoni, moja; lango la Isakari, moja; lango la Zabuloni, moja. 34  “Mpaka wa magharibi utakuwa mikono 4,500, kukiwa na malango matatu, lango la Gadi, moja; lango la Asheri, moja; lango la Naftali, moja. 35  “Kuzunguka pande zote kutakuwa mikono 18,000; na jina la jiji kutoka siku hiyo na kuendelea litakuwa, Yehova Mwenyewe Yupo Hapo.”+

Maelezo ya Chini