Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Biblia Kwenye Mtandao | BIBLIA TAKATIFU--TAFSIRI YA ULIMWENGU MPYA

Ezekieli 40:1-49

40  Katika mwaka wa 25 wa uhamisho+ wetu, mwanzoni mwa mwaka, siku ya 10 ya mwezi, katika mwaka wa 14 baada ya jiji kupigwa na kuangushwa,+ siku hiyohiyo mkono wa Yehova ukawa juu yangu,+ hivi kwamba akanileta mahali hapo.+  Katika maono ya Mungu alinileta katika nchi ya Israeli na hatua kwa hatua akaniweka juu ya mlima mrefu sana,+ ambao juu yake palikuwa na kitu kama muundo wa jiji kuelekea kusini.+  Naye akanileta huko, na, tazama! alikuwapo mtu fulani. Sura yake ilikuwa kama shaba,+ naye alikuwa na kamba ya kitani mkononi mwake, na utete wa kupimia,+ naye alikuwa amesimama langoni.  Naye mtu huyo akaanza kuniambia: “Mwana wa binadamu,+ ona kwa macho yako, na kwa masikio yako usikie, na uweke moyo wako juu ya yote ninayokuonyesha, kwa sababu umeletwa hapa nipate kukuonyesha. Itangazie nyumba ya Israeli kila kitu unachokiona.”+  Na, tazama! kulikuwa na ukuta nje ya nyumba kuizunguka pande zote. Na katika mkono wa mtu huyo kulikuwa na utete wa kupimia wenye urefu wa mikono sita, na wenye kipimo cha mkono mmoja na cha upana wa kiganja kimoja. Naye akaanza kupima upana wa kitu kilichojengwa, utete mmoja; na kimo chake, utete mmoja.  Kisha akaja katika lango, ambalo upande wake wa mbele unaelekea mashariki,+ akapanda juu kwa kutumia ngazi zake. Naye akaanza kupima kizingiti cha lango hilo,+ upana wa utete mmoja, na kile kizingiti kingine, upana wa utete mmoja.  Na chumba cha walinzi kilikuwa na urefu wa utete mmoja na upana wa utete mmoja, na kati ya vyumba vya walinzi+ kulikuwa na kipimo cha mikono mitano; na kizingiti cha lango kando ya ukumbi wa lango kuelekea upande wa ndani kilikuwa utete mmoja.  Naye akapima ukumbi wa lango kuelekea upande wa ndani, utete mmoja.+  Kwa hiyo akapima ukumbi wa lango, mikono minane; na nguzo zake za kando, mikono miwili; na ukumbi wa lango ulielekea upande wa ndani. 10  Na vyumba vya walinzi vya lango kuelekea mashariki vilikuwa vitatu upande huu na vitatu upande ule. Hivyo vitatu vilikuwa na kipimo kilekile, nazo nguzo za kando zilikuwa na kipimo kilekile, upande huu na upande ule. 11  Kisha akapima upana wa mwingilio wa lango, mikono kumi; urefu wa lango, mikono kumi na mitatu. 12  Na eneo lililozungushiwa ua mbele ya vyumba vya walinzi lilikuwa mkono mmoja, na kulikuwa na eneo la mkono mmoja kila upande lililozungushiwa ua. Na chumba cha mlinzi kilikuwa mikono sita upande huu na mikono sita upande ule. 13  Naye akapima lango kutoka kwenye dari ya chumba kimoja cha mlinzi mpaka kwenye dari ya kile kingine, upana wa mikono 25;+ mwingilio mmoja ulielekeana na mwingilio mwingine. 14  Kisha akafanya nguzo za kando za mikono 60, pia nguzo za kando za ua katika malango kuzunguka pande zote. 15  Na upande wa mbele wa lango la njia ya kuingilia mpaka upande wa mbele wa ukumbi wa lango la ndani ulikuwa mikono 50. 16  Na palikuwa na madirisha yenye viunzi vyenye upana tofauti+ kwa ajili ya vyumba vya walinzi na kwa ajili ya nguzo zao za kando kuelekea upande wa ndani wa lango kuzunguka pande zote, na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa ajili ya zile kumbi. Nayo madirisha yalikuwa yenye kuzunguka pande zote kuelekea upande wa ndani, na kwenye nguzo za kando palikuwa na maumbo ya mitende.+ 17  Naye akanileta hatua kwa hatua ndani ya ua wa nje, na, tazama! palikuwa na vyumba vya kulia chakula,+ na sakafu ya mawe iliyofanywa kwa ajili ya ua kuzunguka pande zote. Palikuwa na vyumba 30 vya kulia chakula juu ya ile sakafu ya mawe.+ 18  Nayo sakafu ya mawe kando ya malango ilikuwa sawa kabisa na urefu wa malango—ile sakafu ya chini ya mawe. 19  Naye akapima upana kutoka upande wa mbele wa lango la chini mpaka mbele ya ua wa ndani. Upande wake wa nje ulikuwa mikono mia moja, upande wa mashariki na upande wa kaskazini. 20  Na ua wa nje ulikuwa na lango ambalo upande wake wa mbele ulielekea kaskazini. Akapima urefu wake na upana wake. 21  Navyo vyumba vyake vya walinzi vilikuwa vitatu upande huu na vitatu upande ule. Na nguzo zake za kando na ukumbi wake zilikuwa kulingana na kipimo cha lango la kwanza. Urefu wake mikono 50, na upana wake mikono 25. 22  Na kipimo cha madirisha yake na ukumbi wake na maumbo yake ya mitende+ kilikuwa sawa na kipimo cha lango ambalo upande wake wa mbele unaelekea mashariki. Na kwa kutumia vipandio saba watu wangeweza kupanda kuingia ndani yake, na ukumbi wake ulikuwa mbele yake. 23  Na lango la ua wa ndani lilielekeana na lango la upande wa kaskazini; pia lile la upande wa mashariki. Naye akapima kutoka lango moja mpaka lango lingine mikono mia moja. 24  Naye akanileta hatua kwa hatua upande wa kusini,+ na, tazama! kulikuwa na lango upande wa kusini, naye akapima nguzo zake za kando na ukumbi wake kwa vipimo sawa na hivi. 25  Na palikuwa na madirisha kuzunguka pande zote juu yake na juu ya ukumbi wake, kama madirisha hayo. Urefu wake mikono 50, na upana wake mikono 25. 26  Na palikuwa na ngazi saba za kulipandia, na ukumbi wake ulikuwa mbele yake.+ Nalo lilikuwa na maumbo ya mitende, moja upande huu na lingine upande ule juu ya nguzo zake za kando. 27  Na ua wa ndani ulikuwa na lango upande wa kusini. Naye akapima kutoka lango mpaka lango upande wa kusini mikono mia moja. 28  Naye akanileta hatua kwa hatua mpaka ndani ya ua wa ndani kupitia lango la kusini. Naye akalipima lango la kusini kwa vipimo sawa na hivi. 29  Navyo vyumba vyake vya walinzi na nguzo zake za kando na ukumbi wake vilikuwa na vipimo sawa na hivi. Na palikuwa na madirisha kuzunguka pande zote juu yake na juu ya ukumbi wake. Urefu wake mikono 50, na upana wake mikono 25.+ 30  Na palikuwa na kumbi kuzunguka pande zote; urefu wake mikono 25, na upana wake mikono 5. 31  Na ukumbi wake ulielekea ua wa nje, na maumbo ya mitende yalikuwa kwenye nguzo zake za kando,+ na mpando wake ulikuwa vipandio vinane.+ 32  Naye akanileta hatua kwa hatua ndani ya ua wa ndani kupitia njia ya mashariki, naye akapima lango kwa vipimo sawa na hivi. 33  Navyo vyumba vyake vya walinzi na nguzo zake za kando na ukumbi wake vilikuwa na vipimo sawa na hivi, hilo na ukumbi wake lilikuwa na madirisha kuzunguka pande zote juu. Urefu wake mikono 50, na upana wake mikono 25. 34  Na ukumbi wake ulielekea ua wa nje, na maumbo ya mitende yalikuwa kwenye nguzo zake za kando upande huu na upande ule. Na mpando wake ulikuwa vipandio vinane. 35  Naye akanileta ndani ya lango la kaskazini,+ naye akapima, kwa vipimo sawa na hivi,+ 36  vyumba vyake vya walinzi, nguzo zake za kando na ukumbi wake. Nalo lilikuwa na madirisha kuzunguka pande zote. Urefu wake mikono 50, na upana wake mikono 25. 37  Na kuelekea ua wake wa nje palikuwa na nguzo zake za kando, na maumbo ya mitende yalikuwa juu ya nguzo zake za kando upande huu na upande ule.+ Na mpando wake ulikuwa vipandio vinane. 38  Na chumba cha kulia chakula pamoja na mwingilio wake kilikuwa kando ya nguzo za kando za malango. Hapo ndipo walipokuwa wakioshea toleo zima la kuteketezwa.+ 39  Na katika ukumbi wa lango palikuwa na meza mbili upande huu na meza mbili upande ule, za kuchinjia juu yake lile toleo zima la kuteketezwa+ na lile toleo la dhambi+ na lile toleo la hatia.+ 40  Na upande wa nje, mtu anapopanda mpaka kwenye mwingilio wa lango la kaskazini, palikuwa na meza mbili. Na ule upande mwingine wa ukumbi wa lango palikuwa na meza mbili. 41  Palikuwa na meza nne hapa na meza nne pale kando ya lango—meza nane, ambazo walikuwa wakichinjia juu yake. 42  Na zile meza nne kwa ajili ya toleo zima la kuteketezwa zilikuwa za mawe yaliyochongwa. Urefu wake mkono mmoja na nusu, na upana wake mkono mmoja na nusu, na kimo kilikuwa mkono mmoja. Juu yake pia walikuwa wakiweka vifaa ambavyo walikuwa wakitumia kuchinjia toleo zima la kuteketezwa na ile dhabihu. 43  Na rafu za kuwekea vitu zilikuwa na upana wa kiganja kimoja, zikiwa zimefungwa kwa uthabiti upande wa ndani, kuzunguka pande zote; na juu ya meza walikuwa wakiweka nyama ya toleo la zawadi.+ 44  Na upande wa nje wa lango la ndani palikuwa na vyumba vya kulia chakula vya waimbaji,+ katika ua wa ndani, ulio upande wa lango la kaskazini. Na upande wake wa mbele ulielekea kusini. Palikuwa na kimoja upande wa lango la mashariki. Upande wake wa mbele ulielekea kaskazini. 45  Naye akaniambia: “Hiki, chumba cha kulia chakula ambacho upande wake wa mbele unaelekea kusini, ni cha makuhani wanaotimiza wajibu wa nyumba.+ 46  Na chumba cha kulia chakula ambacho upande wake wa mbele unaelekea kaskazini ni cha makuhani wanaotimiza wajibu wa madhabahu.+ Hao ni wana wa Sadoki,+ ambao, kutoka kwa wana wa Lawi, wanamkaribia Yehova ili kumhudumia.”+ 47  Naye akapima ua wa ndani. Urefu wake ulikuwa mikono 100, na upana mikono 100, mraba. Nayo madhabahu ilikuwa mbele ya nyumba. 48  Naye akanileta ndani ya ukumbi wa nyumba, naye akapima nguzo ya kando ya ukumbi,+ mikono 5 upande huu na mikono 5 upande ule. Na upana wa lango ulikuwa mikono 3 upande huu na mikono 3 upande ule. 49  Urefu wa ukumbi ulikuwa mikono 20, na upana wake mikono 11. Nao walikuwa wakiupanda kwa kutumia ngazi. Na palikuwa na nguzo kando ya miimo ya kando, mmoja hapa na mmoja pale.+

Maelezo ya Chini