Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Ayubu 5:1-27

5  “Ita, tafadhali! Je, kuna yeyote anayekujibu?Nawe utamwendea nani kati ya watakatifu?   Kwa maana usumbufu utamuua mpumbavu,Na mtu anayeshawishiwa kwa urahisi wivu utamuua.   Mimi mwenyewe nimemwona mpumbavu akitia mizizi,+Lakini ghafula nikaanza kuyalaani makao yake.   Wanawe wanakaa mbali na wokovu,+Nao hupondwa langoni bila kuwa na mkombozi.   Kile anachovuna mwenye njaa hukila;Na hata mtu hukichukua kutoka kwenye kulabu za mchinjaji, Na kwa kweli mtego hukamata riziki yao.   Kwa maana madhara hayatoki katika mavumbi matupu,Wala taabu haichipuki katika udongo mtupu.   Kwa maana mwanadamu huzaliwa kwa ajili ya taabu,Kama vile cheche za moto zinavyoruka juu.   Hata hivyo, mimi mwenyewe ningetoa maombi kwa Mungu,Nami ningempelekea Mungu takwa langu,+   Kwake Yeye anayetenda mambo makuu yasiyochunguzika,Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu;+ 10  Kwake Yeye anayenyesha mvua juu ya uso wa dunia+Na kupeleka maji juu ya mashamba;+ 11  Kwake Yeye anayewaweka mahali pa juu wale walio chini,+Hivi kwamba wale walio na huzuni wanakuwa juu katika wokovu; 12  Kwake Yeye anayevunja hila za werevu,Hivi kwamba mikono yao haifanyi kazi ikawa na matokeo;+ 13  Kwake Yeye anayewakamata wenye hekima katika ujanja wao wenyewe,+Hivi kwamba shauri la watu werevu linafanywa haraka-haraka;+ 14  Wanakutana na giza hata wakati wa mchana,Nao wanapapasa-papasa katikati ya mchana kana kwamba ni usiku;+ 15  Na kwake Yeye anayeokoa kutoka kwa upanga unaotoka kinywani mwao,Na maskini kutoka kwa mkono wa mwenye nguvu,+ 16  Hivi kwamba panakuwa na tumaini kwa ajili ya mtu wa hali ya chini,+Lakini ukosefu wa uadilifu kwa kweli hufunga kinywa chake.+ 17  Tazama! Ni mwenye furaha mtu yule ambaye Mungu humkaripia;+Nawe usiikatae nidhamu ya Mweza-Yote! 18  Kwa maana yeye husababisha maumivu, lakini hulifunga jeraha;Yeye huvunja vipande-vipande, lakini mikono yake huponya. 19  Yeye atakukomboa kutoka katika taabu sita,+Na katika saba kitu chochote chenye kudhuru hakitakugusa.+ 20  Yeye atakukomboa kutoka katika kifo wakati wa njaa,+Na kutoka katika nguvu za upanga wakati wa vita. 21  Utafichwa kutoka kwenye pigo la ulimi,+Nawe hutaogopa uporaji unapokuja. 22  Utacheka uporaji na njaa,Wala hutahitaji kuogopa mnyama-mwitu wa dunia. 23  Kwa maana agano lako litakuwa pamoja na mawe ya shambani,Na mnyama wa mwituni atafanywa aishi kwa amani pamoja na wewe.+ 24  Nawe hakika utajua kwamba amani ndiyo hema lako,Nawe bila shaka utaenda kuyaona malisho yako, wala hutakosa chochote. 25  Nawe hakika utajua kuwa uzao wako ni mwingi+Na wazao wako kama majani ya dunia.+ 26  Utaingia kaburini ukiwa na nguvu,+Kama wakati miganda inaporundikana wakati wake. 27  Tazama! Hayo ndiyo tumeyachunguza. Na ndivyo yalivyo.Uyasikie, nawe—uyajue kwa ajili yako mwenyewe.”

Maelezo ya Chini