Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Ayubu 41:1-34

41  “Je, unaweza kumvua Lewiathani*+ kwa ndoano,Au, je, unaweza kuufunga ulimi wake kwa kamba?   Je, unaweza kutia kitete katika pua yake,+Au, je, unaweza kutoboa taya zake kwa mwiba?   Je, atakusihi wewe sana,Au, je, atakuambia maneno ya upole?   Je, atafanya agano pamoja nawe,Ili umfanye kuwa mtumwa mpaka wakati usio na kipimo?   Je, utamchezea kama ndege,Au, je, utamfunga kwa ajili ya wasichana wako wadogo?   Je, rafiki watafanya biashara juu yake?Je, watamgawanya yeye katikati ya wafanya-biashara?   Je, utajaza vyuma vyenye ncha+ katika ngozi yake,Au kujaza mikuki ya samaki katika kichwa chake?   Tia mkono wako juu yake.Kumbuka pigano hilo. Usifanye hivyo tena.   Tazama! Matarajio ya mtu kumhusu hakika yatakatishwa tamaa.Mtu pia ataangushwa chini kwa kule kumwona tu. 10  Hakuna aliye na ushupavu kiasi cha kumwamsha.Na ni nani ambaye anaweza kusimama mbele zangu?+ 11  Ni nani ambaye amenipa kitu kwanza, ndipo nilazimike kumpa thawabu?+Vitu vyote ni vyangu chini ya mbingu zote.+ 12  Sitanyamaza kimya kuhusu sehemu zakeAu habari ya nguvu zake na uzuri wa vipimo vyake. 13  Ni nani ambaye ameufunua uso wa mavazi yake?Ni nani anayeweza kuingia ndani ya taya zake mbili? 14  Ni nani amepata kuifungua milango ya uso wake?Meno yake kuzunguka pande zote ni yenye kuogopesha. 15  Mitaro ya magamba ndiyo majivuno yake,Yaliyofungwa kana kwamba kwa muhuri uliokazwa. 16  Hayo huingiana yenyewe karibu-karibu,Na hata hewa haiwezi kuingia katikati yake. 17  Yamefungamana kila moja na lingine;Yanashikamana wala hayawezi kutenganishwa. 18  Chafya zake huangaza nuru,Na macho yake ni kama miali ya mapambazuko. 19  Miwako ya umeme hutoka katika kinywa chake,Hata cheche za moto hutoka. 20  Moshi hutoka katika mianzi ya pua yake,Kama tanuru iliyowashwa moto kwa matete. 21  Nafsi yake huwasha moto makaa,Na mwali wa moto hutoka katika kinywa chake. 22  Nguvu zinakaa katika shingo yake,Na ukataji tamaa hukimbia mbele yake. 23  Makunjo ya nyama yake hushikamana pamoja;Hayo ni kama kitu kilichoundwa katika kalibu juu yake, kisichoondoleka. 24  Moyo wake umetengenezwa kama jiwe,Ndiyo, umetengenezwa kama jiwe la chini la kusagia. 25  Wenye nguvu huingiwa na woga kwa sababu ya kuinuka kwake;+Wao hutatanishwa na fadhaa. 26  Upanga ukimfikia haumwezi,Wala mkuki, kishale wala ncha ya mshale.+ 27  Yeye huona chuma+ kuwa kama nyasi tu,Shaba kuwa kama mti uliooza. 28  Mshale haumfukuzi;Kwake mawe ya kombeo+ yamebadilishwa kuwa majani makavu. 29  Yeye huiona rungu kuwa kama tu majani makavu,+Naye huucheka mtikiso wa mkuki. 30  Sehemu zake za chini ni kama vigae vilivyochongoka;Yeye hujinyoosha kama kifaa cha kupuria+ juu ya matope. 31  Yeye huvichemsha vilindi kama chungu;Huifanya bahari iwe kama chungu cha marhamu. 32  Hufanya njia ing’ae nyuma yake;Mtu atafikiri kilindi cha maji ni kichwa chenye mvi. 33  Hakuna aliye kama yeye juu ya mavumbi,Yeye aliyefanywa asiweze kutishika. 34  Yeye huona kila kitu kilicho juu.Yeye ni mfalme juu ya wanyama-mwitu wote wenye fahari.”

Maelezo ya Chini

Au mamba.