Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Ayubu 26:1-14

26  Naye Ayubu akajibu, akasema:   “Lo! Jinsi umekuwa msaada kwa mtu asiye na uwezo!Lo! Jinsi umeokoa mkono usio na nguvu!+   Jinsi umemshauri mtu asiye na hekima,+Nawe umefanya umati ujue hekima inayotumika!   Umemwambia nani maneno,Na ni pumzi ya nani imetoka kwako?   Wale wasiojiweza katika kifo wanaendelea kutetemekaChini ya maji na wale wanaokaa ndani yake.+   Kaburi* liko uchi mbele zake,+Na mahali pa maangamizi hapana kifuniko.   Anaitandaza kaskazini juu ya mahali pasipo na kitu,+Akiitundika dunia pasipo na kitu;   Anafunga maji katika mawingu yake,+Hivi kwamba wingu kubwa halipasuki chini yayo;   Anaufunika uso wa kiti cha ufalme,Anatandaza juu yake wingu lake.+ 10  Amechora mviringo juu ya uso wa maji,+Mpaka mahali ambapo nuru huishia katika giza. 11  Nguzo za mbingu hutikisika,Nazo hushangaa kwa sababu ya kemeo lake. 12  Kwa uwezo wake ameichochea bahari,+Naye kwa uelewaji wake amemvunja vipande-vipande+ yule mshambuliaji.+ 13  Kwa upepo wake ameng’arisha mbingu,+Mkono wake umemchoma yule nyoka anayenyiririka.+ 14  Tazama! Hizo ndizo kingo za njia zake,+Nao ni mnong’ono ulioje wa jambo lililosikiwa juu yake!Lakini kuhusu mngurumo wake wenye nguvu ni nani anayeweza kuonyesha uelewaji?”+

Maelezo ya Chini

Sheoli. Tazama Nyongeza 4.