Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Biblia Kwenye Mtandao | BIBLIA TAKATIFU—TAFSIRI YA ULIMWENGU MPYA (TOLEO LA 2003) Ona toleo la 2017

Ayubu 18:1-21

18  Naye Bildadi Mshua akajibu, akasema:   “Ninyi mtachukua muda gani ili kukomesha maneno?Mnapaswa kuelewa, ili baadaye tuseme.   Kwa nini tuhesabiwe kuwa wanyama+Na kuonwa kuwa wasio safi machoni penu?   Yeye anararua vipande-vipande nafsi yake katika hasira yake.Je, dunia iachwe kwa ajili yako,Au jiwe liondoke mahali pake?   Pia nuru ya waovu itazimwa+Na cheche ya moto wake haitang’aa.   Hakika nuru itafifia katika hema lake,+Na humo taa yake itazimwa.   Hatua zake zenye nguvu zitasongwa.Hata shauri lake litamtupilia mbali.+   Kwa maana miguu yake itamwingiza ndani ya wavu,Naye atatembea kwenye kamba za wavu.+   Mtego utamkamata kisigino;+Mnaso+ unaendelea kumkamata. 10  Kamba imefichwa katika udongo kwa ajili yake,Na kwa ajili yake chombo cha kunasia katika njia yake. 11  Pande zote, hofu za ghafula hakika zinamshtua kwa woga,+Na kwelikweli kumfukuza miguuni pake. 12  Nguvu zake zinaliwa na njaa,Na msiba+ husimama tayari ili kumfanya achechemee. 13  Utakula vipande vya ngozi yake;Mzaliwa wa kwanza wa kifo atakula viungo vyake. 14  Uhakika wake utaondolewa katika hema lake+Nayo itampeleka kwa mfalme wa hofu. 15  Ndani ya hema lake kitakaa kitu ambacho si chake;Kiberiti+ kitatawanywa juu ya makao yake. 16  Chini, mizizi yake itakauka,+Na juu, tawi lake litanyauka. 17  Kutajwa kwake hakika kutaangamia kutoka duniani,+Wala hatakuwa na jina lolote nje barabarani. 18  Watamsukuma kutoka nuruni kuingia gizani,Nao watamfukuza kutoka katika nchi yenye kuzaa. 19  Hatakuwa na wazao wala watoto katikati ya watu wake,+Wala hapatakuwa na mwokokaji mahali pake pa makao ya kigeni. 20  Watu walio Magharibi wataiangalia siku yake kwa mshangao,Na hata watu walio Mashariki watashikwa na mtetemeko. 21  Ila tu hizo ndizo maskani za mkosaji,Na hapa ndipo mahali pa mtu ambaye hajamjua Mungu.”

Maelezo ya Chini