Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Ayubu 15:1-35

15  Naye Elifazi Mtemani akajibu, akasema:   “Je, mtu mwenye hekima atajibu kwa ujuzi wa upepo,+Au, je, atalijaza tumbo lake upepo wa mashariki?+   Kukaripia tu kwa neno hakutakuwa na faida yoyote,Na maneno matupu peke yake hayatakuwa na faida.   Hata hivyo, wewe mwenyewe unafanya woga mbele za Mungu usiwe na nguvu zozote,Nawe unapunguza kuwa na hangaiko lolote mbele za Mungu.   Kwa maana kosa lako linakizoeza kinywa chako,Nawe unachagua ulimi wa watu werevu.   Kinywa chako kinakutangaza wewe kuwa mwovu, wala si mimi;Na midomo yako mwenyewe inajibu juu yako.+   Je, wewe ndiye mwanadamu wa kwanza kabisa kuzaliwa,+Au, je, ulizaliwa kwa uchungu kabla ya vilima?+   Je, wewe husikiliza mazungumzo ya siri ya Mungu,+Na je, ni wewe peke yako mwenye hekima?   Kwa kweli unajua nini ambacho sisi hatujui?+Unaelewa nini ambacho sisi hatuna pia? 10  Mwenye kichwa chenye mvi na mzee pia, wote wapo pamoja nasi,+Yeye aliye na siku nyingi kuliko baba yako. 11  Je, faraja za Mungu hazikutoshi wewe,Au neno uliloambiwa kwa upole? 12  Kwa nini yaliyo moyoni mwako yanakuchukua,Na kwa nini macho yako yanawaka? 13  Kwa maana wewe unaigeuza roho yako kinyume cha Mungu mwenyewe,Nawe umeyatokeza maneno katika kinywa chako mwenyewe. 14  Mwanadamu anayeweza kufa ni nani ndipo awe safi,+Au ndipo yeyote aliyezaliwa na mwanamke awe upande wa haki? 15  Tazama! Yeye hana imani na watakatifu wake,+Na mbingu zenyewe kwa kweli si safi machoni pake.+ 16  Sembuse mtu anayechukiza na aliye mpotovu,+Mtu anayekunywa ukosefu wa uadilifu kama maji! 17  Nitakutangazia. Wewe nisikilize!+Nimeona hata jambo hili, basi acha nilisimulie, 18  Lile ambalo watu wenye hekima+ wenyewe hulisemaNa ambalo hawakuficha, hilo likiwa limetoka kwa baba zao. 19  Wao peke yao walipewa nchi hiyo,Wala hakuna mgeni aliyepita katikati yao. 20  Mwovu anapata mateso siku zake zote,Pia hesabu ya miaka ambayo imewekewa mwonevu. 21  Sauti ya vitu vyenye kutia hofu imo masikioni mwake;Mporaji huja juu yake wakati wa amani.+ 22  Hasadiki kwamba atarudi kutoka katika giza,+Naye amewekwa kwa ajili ya upanga. 23  Anapotea njia akitafuta mkate—uko wapi?+Anajua vema kwamba siku ya giza+ iko tayari mkononi mwake. 24  Taabu na maumivu huendelea kumtia hofu;+Humshinda nguvu kama mfalme aliyejitayarisha kwa ajili ya shambulio. 25  Kwa sababu yeye ananyoosha mkono wake juu ya Mungu mwenyewe,Naye anajaribu kujionyesha kuwa mkuu juu ya Mweza-Yote;+ 26  Kwa sababu anakimbia juu yake kwa ugumu wa shingo,Na vinundu vizito vya ngao zake; 27  Kwa sababu yeye kwa kweli anafunika uso wake kwa wingi wa mafuta yakeNaye anaongeza mafuta juu ya viuno vyake,+ 28  Anakaa tu katika majiji ambayo yatafutiliwa mbali;Katika nyumba ambamo watu hawataendelea kukaa,Ambazo kwa hakika zimekusudiwa kuwa marundo ya mawe. 29  Yeye hatatajirika wala mali yake haitaongezeka,Wala hatatandaza mapato yao juu ya dunia.+ 30  Yeye hatageuka kutoka gizani;Mwali wa moto utakausha tawi lake,Naye atageuka kando kwa mlipuko wa kinywa chake Yeye.+ 31  Na asiwe na imani katika ubatili, akiwa anapotoshwa,Kwa maana badala yake atapata ubatili mtupu; 32  Itatimizwa kabla ya siku yake.Na chipukizi lake halitakuwa na majani mengi.+ 33  Atatupa zabibu zake mbichi kama mzabibu,Na kutupilia mbali maua yake kama mzeituni. 34  Kwa maana kusanyiko la waasi-imani ni tasa,+Na moto wenyewe utayateketeza mahema ya rushwa.+ 35  Taabu inatungwa mimba na mambo yenye kudhuru yanazaliwa,+Nalo tumbo lao hutayarisha udanganyifu.”

Maelezo ya Chini