Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Biblia Kwenye Mtandao | BIBLIA TAKATIFU—TAFSIRI YA ULIMWENGU MPYA (TOLEO LA 2003) Ona toleo la 2017

1 Samweli 27:1-12

27  Hata hivyo, Daudi akasema moyoni mwake: “Sasa mkono wa Sauli utanifagilia mbali siku moja. Hakuna jambo bora kwangu kuliko kuponyoka+ bila shaka, niende katika nchi ya Wafilisti;+ na Sauli atakata tamaa ya kunitafuta tena katika eneo lote la Israeli,+ nami nitaponyoka kutoka mkononi mwake.”  Basi Daudi akaondoka, yeye pamoja na watu mia sita+ waliokuwa pamoja naye, akavuka kwenda kwa Akishi+ mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi.  Na Daudi akaendelea kukaa na Akishi katika Gathi, yeye pamoja na watu wake, kila mmoja na nyumba yake,+ Daudi na wake zake wawili, Ahinoamu+ Myezreeli na Abigaili,+ mke wa Nabali Mkarmeli.  Baada ya muda Sauli akapelekewa habari kwamba Daudi alikuwa amekimbia kwenda Gathi, kwa hiyo hakwenda kumtafuta tena.+  Ndipo Daudi akamwambia Akishi: “Ikiwa sasa nimepata kibali machoni pako, na wanipe mahali katika moja la majiji ya mashambani, ili nikae huko; kwa nini mtumishi wako akae katika jiji la kifalme pamoja nawe?”  Basi Akishi akampa Siklagi+ siku hiyo. Ndiyo sababu Siklagi limekuwa la wafalme wa Yuda mpaka leo hii.  Na hesabu ya siku ambazo Daudi alikaa katika nchi ya mashambani ya Wafilisti ikawa mwaka mmoja na miezi minne.+  Na Daudi akapanda pamoja na watu wake ili wavamie Wageshuri+ na Wagirzi na Waamaleki;+ kwa maana walikuwa wakikaa katika nchi iliyoanzia Telamu+ mpaka Shuri+ na kushuka mpaka nchi ya Misri.  Naye Daudi akaipiga nchi, lakini hakuhifadhi hai mwanamume wala mwanamke;+ naye akachukua makundi na mifugo na punda na ngamia na mavazi, kisha akarudi, akaja kwa Akishi. 10  Ndipo Akishi akasema: “Mlivamia wapi leo?” Naye Daudi akasema:+ “Upande wa kusini wa Yuda+ na upande wa kusini wa Wayerahmeeli+ na upande wa kusini wa Wakeni.”+ 11  Na kuhusu mwanamume na mwanamke, Daudi hakuhifadhi hai yeyote ili kuwaleta Gathi, akisema: “Wasije wakatusema kwa maneno haya, ‘Hivi ndivyo Daudi alivyofanya.’”+ (Na hii imekuwa kawaida yake siku zote ambazo aliishi katika nchi ya mashambani ya Wafilisti.) 12  Kwa hiyo Akishi akamwamini+ Daudi, akisema moyoni mwake: “Bila shaka amenuka katikati ya watu wake Israeli;+ naye atakuwa mtumishi wangu mpaka wakati usio na kipimo.”

Maelezo ya Chini