Aprili 5, 2017, Mahakama Kuu itasikiliza kesi kuhusu kuwapiga marufuku Mashahidi wa Yehova nchini Urusi. Kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, Vasiliy Kalin, mwakilishi wa Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi, anawasihi wenye mamlaka serikalini wakomeshe mateso yasiyo ya haki dhidi ya Mashahidi wa Yehova. Taarifa yake iliwekwa kwenye tovuti ya jw-russia.org mnamo Machi 21, 2017.