Julai 14, 2015, maofisa wa forodha wa Urusi walichukua hatua kali sana kuelekea Mashahidi wa Yehova kwa kuzuia kuingizwa kwa Biblia ya Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Maandiko Matakatifu, iliyochapishwa na Mashahidi katika Kirusi. Tangu Machi 2015, wenye mamlaka nchini Urusi wamezuia mizigo ya machapisho ya kidini ya Mashahidi, hata ingawa katika mizigo hiyo hakuna machapisho yoyote yaliyopigwa marufuku nchini Urusi. Inatia hofu kwamba wenye mamlaka wamezuia kuingizwa kwa machapisho nchini humo na hivi karibuni wamepiga marufuku tovuti rasmi ya www.jw.org, hatua ambayo inazuia uhuru wa ibada, uhuru wa usemi na uhuru wa vyombo vya habari.