Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JUNI 1, 2015
URUSI

Uamuzi Muhimu Katika Kesi ya Taganrog Watarajiwa Kutolewa Karibuni

Uamuzi Muhimu Katika Kesi ya Taganrog Watarajiwa Kutolewa Karibuni

Kesi inayosikilizwa upya ya Mashahidi 16 wa Yehova jijini Taganrog, Urusi, iko katika mwezi wake watano tangu ilipoanza kusikilizwa Februari 2015. Ikiwa watashindwa, watahukumiwa vifungo na faini kwa sababu ya kutenda kupatana na imani yao.

Kesi yao ilianza Mei 13, 2013, baada ya kuhukumiwa kwa kosa la kujihusisha katika vitendo vinavyoonwa kuwa vyenye msimamo mkali. Mahakama iliwatoza faini Mashahidi saba na wanne walihukumiwa vifungo vya muda mrefu gerezani, lakini hakimu alisitisha hukumu hizo. Desemba 12, 2014, kwa ombi la mwendesha-mashtaka, mahakama ya rufaa iliagiza kesi hiyo isikilizwe tena upya. Mashahidi wa Yehova wanatarajia hukumu mpya kufikia mwishoni mwa mwezi wa Juni.