Kesi ya uhalifu dhidi ya Mashahidi wa Yehova katika eneo la Taganrog, ni mojawapo ya matukio mengi yanayoongezeka ya upinzani wa kidini nchini Urusi. Hakimu wa kesi hiyo atatoa hukumu hivi karibuni. Je, Urusi itawafunga wananchi wake kwa sababu tu ya imani yao isiyovuruga amani? Video hii ina maelezo yaliyotolewa na Bw. Gajus Glockentin, msemaji wa European Association of Jehovah’s Witnesses, yanayotoa himizo la kuheshimu haki na uhuru wa dini.