Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

AGOSTI 2, 2017
URUSI

Maoni ya Mataifa Mbalimbali Kuhusu Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

Maoni ya Mataifa Mbalimbali Kuhusu Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

Mashirika na maofisa wa mataifa mbalimbali wameeleza maoni yao kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi wa kuipiga marufuku ibada ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi. Maelezo haya yamechambua uamuzi wa mahakama usio wa haki wa Urusi na uliopita kiasi dhidi ya kikundi cha kidini chenye waabudu wachache ambacho kinajulikana kwa kufanya utendaji wao wa kidini kwa amani.

Julai 17, 2017, majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Rufaa ya Urusi waliunga mkono uamuzi wa awali wa mahakama uliotolewa Aprili 20 ambao “ulipiga marufuku shirika la kidini la ‘Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi’ na mashirika ya kidini ambayo ni sehemu ya Kituo hicho cha usimamizi na kutaifisha mali zote za shirika hilo kuwa mali za Shirikisho la Urusi.” Kwa uamuzi huo, Mahakama imepiga marufuku ibada ya Mashahidi wa Yehova katika nchi nzima ya Urusi.

Maelezo Baada ya Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa wa Julai 17, 2017

Yafuatayo ni sehemu za maelezo yaliyotolewa baada ya uamuzi wa Julai 17, 2017 wa Mahakama Kuu ya Rufaa ya Urusi ambao uliounga mkono uamuzi wa Aprili 20:

“Tunasikitishwa sana na uamuzi wa Mahakama Kuu wa kukataa rufaa ya Mashahidi wa Yehova kuhusu kutangazwa kuwa na ‘msimamo mkali.’ Uamuzi huo unathibitisha wazi kwamba ibada inayofanywa kwa amani na raia 175,000 wa Urusi inafanywa kuwa ni uhalifu na unavunja haki ya uhuru wa kuabudu ambayo inatetewa na Katiba ya Urusi.”—Lord Ahmad wa Wimbledon, Waziri wa Mambo ya Nje wa Haki za Kibinadamu na Ofisi ya Jumuiya ya Madola, Uingereza. https://www.gov.uk/government/news/minister-for-human-rights-statement-on-russian-supreme-court-ruling

“Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi wa juma hili dhidi ya Mashahidi wa Yehova ni mfululizo wa mateso yanayofanywa dhidi ya dini zenye waabudu wachache nchini Urusi. Tunawasihi wenye mamlaka nchini Urusi waondoe marufuku dhidi ya utendaji wa Mashahidi wa Yehova, wafungue Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova, na kumwachilia mshiriki yeyote wa dini zenye waabudu wachache ambaye anaendelea kushikiliwa isivyo haki na wenye mamlaka kwa kile kinachodaiwa kuwa kufanya utendaji ‘wenye msimamo mkali.’”—Heather Nauert, Msemaji wa Idara ya Taifa Nchini Marekani. https://www.state.gov/r/pa/prs/ps/2017/07/272679.htm

“Mashahidi wa Yehova wanapaswa kufurahia uhuru wa kukutanika pamoja kama vikundi vingine vya kidini, uhuru ambao unaelezwa katika Katiba ya Shirikisho la Urusi, pamoja na mikataba ya kimataifa iliyofanywa na Urusi na kulingana na viwango vya haki za kibinadamu za kimataifa.”—Msemaji wa European Union External Action Services. https://eeas.europa.eu/headquarters/headquarters-homepage/30022/statement-spokesperson-upheld-ban-activities-jehovahs-witnesses-russia_en

“Kwa kusikitisha uamuzi wa Mahakama Kuu unaonyesha mtazamo wa serikali wa kufanya ziwe sawa shughuli zinazofanywa kwa amani za uhuru wa kuabudu zionekane kuwa msimamo mkali. Mashahidi si kikundi chenye msimamo mkali, na wanapaswa kufanya utendaji wa imani yao hadharani na kwa uhuru bila kuzuiwa na serikali.”Daniel Mark, Mwenyekiti wa Tume ya Uhuru wa Ibada wa Kimataifa ya Marekani. http://www.uscirf.gov/news-room/press-releases/russia-jehovah-s-witnesses-banned-after-supreme-court-rejects-appeals

“Ninasikitishwa sana kwamba marufuku iliyotolewa na mahakama dhidi ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi imeungwa mkono na mahakama ya rufaa. Licha ya kuwasihi kwa njia mbalimbali, uamuzi huo umefanya uhuru wa ibada na mawazo unaofurahiwa kwa amani uwe kosa la jinai.”—Gernot Erler, Mratibu wa Intersocietal Cooperation With Russia, Central Asia, and the Eastern Partnership Countries, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani. http://www.auswaertiges-amt.de/sid_5DAC942B7DE50BCC4AFCDFC864C2E383/EN/Infoservice/Presse/Meldungen/2017/170719-Ko_RUS-Zeugen_Jehovas.html

“Uamuzi wenye kuaibisha uliofanywa karibuni na Urusi wa kupiga marufuku Mashahidi wa Yehova ili wasitambuliwe kama kikundi cha kidini nchini Urusi ni ukiukwaji mkubwa wa ulinzi wa uhuru wa ibada na imani kama inavyoonyeshwa kwenye kifungu cha 18 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu. . . . Watu wenye mtazamo mzuri kutoka katika kila jamii pamoja na wale wote wanaothamini haki ya uhuru wa dhamiri wanapaswa kuwaunga mkono Mashahidi wa Yehova wa Urusi.”—Dakt. Katrina Lantos Swett, rais, Taasisi ya Lantos. https://www.lantosfoundation.org/news/2017/7/17/lantos-foundation-condemns-russias-outrageous-decision-to-ban-jehovahs-witnesses

Maelezo Baada ya Uamuzi wa Aprili 20, 2017, wa Mahakama Kuu

Kabla ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa, mashirika na maofisa wengi wa serikali mbalimbali waliulaani uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi wa Aprili 20:

“Ninamwomba Rais Vladimir Putin atumie mamlaka yake kuhakikisha haki ya vikundi vyenye waabudu wachache pamoja na Mashahidi wa Yehova.”—Waziri mkuu wa Ujerumani, Angela Merkel, wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais Putin. http://uk.reuters.com/article/uk-russia-germany-putin-syria-idUKKBN17Y1JZ

“Uamuzi wa karibuni wa Mahakama Kuu wa kutangaza Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi kuwa ni shirika lenye msimamo mkali, na kukifunga na kuyafunga mashirika 395 yanayotumiwa na Mashahidi, kumetokeza hangaiko zito kuhusu uhuru wa ibada nchini Urusi na ni mfano wa kutungwa kwa sheria dhidi ya msimamo mkali ambayo inatumiwa isivyo haki kuzuia uhuru wa kujieleza na kukusanyika.”—Theodora Bakoyannis na Liliane Maury Pasquier, wasemaji wa PACE Monitoring Committee kwa ajili ya Shirikisho la Urusi. http://assembly.coe.int/nw/xml/News/News-View-EN.asp?newsid=6599

“Kukataa kuheshimu uhuru wa ibada nchini Urusi ni ukiukwaji mwingine usiovumilika wa mkataba unaofanywa na shirika la OSCE la Moscow [Shirika la Usalama na Ushirikiano Barani Ulaya]. Watu wanaofanya mambo ya kidini kwa amani hawapaswi kuwa katika hatari ya kutendewa vibaya, kutozwa faini, au kufungwa. Amri ya mahakama ya kutaifisha mali zinazomilikiwa na shirika la Mashahidi wa Yehova kumefanya hali iwe mbaya zaidi. Ninatumaini kwamba Mashahidi watakata rufaa na kupeleka kesi hii kwenye Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu.”—Seneta Roger Wicker, Mwenyekiti wa Tume ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya. http://csce.emailnewsletter.us/mail/util.cfm?gpiv=2100141660.2454.614

“Uamuzi uliotolewa jana na Mahakama Kuu ya Urusi wa kupiga marufuku utendaji wa Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi kwa misingi ya ‘msimamo mkali’ kunaweza kufanya iwe rahisi kwa Mashahidi wa Yehova kufunguliwa mashtaka ya uhalifu kwa sababu tu ya kushiriki katika ibada. Kama vikundi vingine vyote vya kidini, Mashahidi wa Yehova wanapaswa kufurahia kukusanyika kwa uhuru na amani bila kuzuiwa, kama Katiba ya Shirikisho la Urusi inavyoonyesha, pamoja na mikataba ya kimataifa ambayo Urusi ni mwanachama na kupatana na viwango vya kimataifa vya haki za kibinadamu.”—Msemaji wa European Union External Action Services. https://eeas.europa.eu/headquarters/headquarters-homepage/24870/statement-ban-activities-jeho

“Ninasikitishwa sana na kitendo cha kuufanya utendaji wenye amani wa Mashahidi wa Yehova nchini Urusi kuwa wa kihalifu bila sababu za msingi. Kitendo hicho ni kuiondoa jamii hii ambayo imekuwapo nchini. Uamuzi wa Mahakama Kuu umetishia viwango na kanuni zinazofanya kuwe na demokrasia, uhuru, uwazi, na jamii kuamini au kuvumilia imani za wengine.”—Michael Georg Link, Msimamizi wa OSCE Ofisi ya Taasisi za Demokrasia na Haki za Binadamu. http://www.osce.org/odihr/313561

“Marufuku hii inawatesa watu wanaofanya amani kwa sababu tu ya kushiriki katika ibada; ni wazi inakiuka haki za msingi za uhuru wa ibada na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu ambavyo Katiba ya Urusi inavikubali. Hii marufuku inapaswa kuondolewa haraka iwezekanavyo.”—Profesa Ingeborg Gabriel, Personal Representative of the OSCE Chairperson-in-Office on Combating Racism, Xenophobia, and Discrimination. http://www.osce.org/odihr/313561

“Nilishtushwa na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi wa kuwaona Mashahidi wa Yehova kuwa na ‘msimamo mkali.’ Uamuzi huo unawazuia raia 175,000 wa Urusi kufanya kwa amani ibada na inakiuka haki ya uhuru wa ibada ambayo ni sehemu ya msingi ya Katiba ya Urusi. Uingereza imeipigia simu serikali ya Urusi ili ishikamane na mikataba ya kimataifa kuhusiana na uhuru.”—Baroness Joyce Anelay, former Minister of State for the Commonwealth and the UN at the Foreign and Commonwealth Office. https://www.gov.uk/government/news/minister-for-human-rights-criticises-russian-supreme-court-ruling-for-labelling-jehovahs-witnesses-as-extremist

Mashirika ya Kimataifa Yashutumu Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi

Julai 20, 2017, Halmashauri ya Kudumu ya OSCE ilituma ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (EU). Ujumbe huo uliitaka Urusi iwaruhusu Mashahidi wa Yehova “waweze kufurahia uhuru wa kukusanyika pamoja kwa amani bila kuingiliwa, kama inavyotakiwa na Katiba ya Urusi na mikataba ya kimataifa ambayo Urusi inaikubali pamoja na viwango vya kimataifa vya haki za kibinadamu.” Washiriki wote 28 wa nchi za Umoja wa Ulaya na nchi nyingine ambazo si washiriki wa Umoja wa Ulaya kama vile Australia, Kanada, na Norway ambazo zimeunga mkono wazo la Umoja wa Ulaya walikubali ujumbe huo utumwe walipokutana jijini Vienna. https://eeas.europa.eu/sites/eeas/files/pc_1155_eu_jehovahs_witnesses_in_russia.pdf

Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote wamesikitishwa sana na uamuzi usio wa haki wa Mahakama Kuu wa kupiga marufuku ibada yao katika nchi nzima. Kwa upande mwingine, taasisi mbalimbali za kimataifa na maofisa mbalimbali wameonyesha wazi kwamba Urusi imekiuka haki kwa kuwatangaza Mashahidi wa Yehova kuwa “wana msimamo mkali” na kwa kukiuka katiba yao wenyewe na mikataba ya kimataifa ambayo inalinda uhuru wa ibada. Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu ipo tayari kusikiliza jambo hili na tunatumaini itaondoa marufuku iliyopigwa nchini humo.