Mei 27, 2015, Wizara ya Sheria ya Shirikisho la Urusi ilisajili shirika la kisheria la Mashahidi wa Yehova la Moscow. Usajili huo umefanyika karibu miaka mitano baada ya Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) kueleza kwamba uamuzi wa mahakama ya Moscow wa kufunga shirika la kisheria la Mashahidi haukuwa halali.

Baada ya miaka mingi ya kufuata taratibu za kisheria, Mahakama ya Wilaya ya Golovinskiy jijini Moscow, ilitoa uamuzi wa kufunga shirika hilo la kisheria la Mashahidi mwaka wa 2004. Mwaka wa 2010, ECHR iliagiza Urusi irekebishe ukosefu huo wa haki kwa kusajili upya shirika hilo na kulilipa fidia. Serikali ya Urusi ililipa faini hiyo lakini sasa ndiyo imetoa usajili huo.