Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

SEPTEMBA 27, 2016
URUSI

Kesi ya Kufunga Makao Makuu ya Mashahidi wa Yehova Nchini Urusi Yaahirishwa Tena

Kesi ya Kufunga Makao Makuu ya Mashahidi wa Yehova Nchini Urusi Yaahirishwa Tena

Septemba 23, 2016, Mahakama ya Wilaya ya Tver jijini Moscow iliahirisha kusikizwa kwa rufani ya Mashahidi dhidi ya onyo linalotishia kufunga Makao Makuu ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi. Zikiwa zimebaki siku tatu tu kabla ya kesi hiyo kusikizwa, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka iliwasilisha malalamiko kwenye mahakama pamoja na habari iliyo na zaidi ya kurasa 200. Mashahidi waliomba wapewe muda ili wazipitie hati hizo, na hakimu akaamua kwamba kesi itasikizwa tena Oktoba 12, 2016. Mahakama hiyo itachunguza rufani ya Mashahidi na pia ikiwa onyo lililotolewa dhidi ya Kituo hicho cha Usimamizi lilizingatia sheria.