Hamia kwenye habari

FEBRUARI 16, 2018
URUSI

Mahakama Jijini Oryol Itaanza Kusikiliza Kesi ya Dennis Christensen Hivi Karibuni

Kesi inayomhusu Dennis Christensen itaanza kusikilizwa Februari 19, 2018. Bw. Christensen, raia wa Denmark na Shahidi wa Yehova, amekuwa mahabusu tangu alipokamatwa mnamo Mei 2017, huko Oryol, Urusi.

Januari 31, 2018, Mwendesha-Mashtaka Msaidizi wa eneo la Oryol alifungua mashtaka yaliyoandikwa kwenye kurasa 76 dhidi ya Bw. Christensen. Mwendesha-Mashtaka alimshtaki kwa kutegemea Sheria ya Uhalifu ya 282.2(1) ya Urusi— kwa kupanga utendaji wa shirika la kidini ambalo lilikuwa limetangazwa kwamba lina msimamo mkali. Hukumu kali zaidi ya kosa hilo inayoweza kutolewa ni kifungo cha miaka kumi gerezani.

Bw. Christensen hana hatia ya uhalifu. Alikamatwa alipokuwa akihudhuria mkutano wa kidini uliofanywa kwa amani akiwa pamoja na mke wake na waabudu wenzake. Kesi itaanza kusikilizwa saa 8:30 mchana, Februari 19, 2018, katika Mahakama ya Wilaya ya Zheleznodorozhniy jijini Oryol.