Hamia kwenye habari

MACHI 1, 2018
URUSI

Mahakama ya Oryol Itaendelea Kusikiliza Kesi ya Dennis Christensen Aprili 3, 2018

Februari 19, 2018, kesi ya uhalifu inayomkabili Dennis Christensen imeanza kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Zheleznodorozhniy jijini Oryol. Watu wengi wanaomuunga mkono Bw. Christensen walifika mahakamani. Pia, balozi wa Ubalozi wa Denmark nchini Urusi, anayeitwa Jeanne Christina Demirci, alikuwa miongoni mwa wale waliofika mahakamani; yeye alisafiri kutoka Moscow ili kuja kusikiliza kesi hiyo. Katika kikao kilichoendelea kwa saa moja tu, Hakimu Aleksey Rudnev alikubali maombi ya Bw. Christensen na mawakili wake ya kupewa muda wa kutosha kuchunguza maandishi ya kesi hiyo. Kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, Mahakama ya Wilaya ya Sovetskiy ilikuwa imemnyima haki hiyo, ilimpatia muda wa majuma mawili tu ili apitie maandishi yote ya kesi hiyo yaliyo na kurasa 2,500 ambayo yalikuwa katika lugha ya Kirusi. Hakimu Rudnev amepanga kesi hiyo ya uhalifu isikilizwe tena Aprili 3, 2018, saa 04:30 asubuhi. Kwa sasa, Bw. Christensen bado yuko mahabusu.