Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

SEPTEMBA 15, 2015
URUSI

Kusikilizwa Upya kwa Kesi ya Mashahidi wa Yehova Jijini Taganrog—Ukosefu wa Haki Utakwisha Lini?

Kusikilizwa Upya kwa Kesi ya Mashahidi wa Yehova Jijini Taganrog—Ukosefu wa Haki Utakwisha Lini?

Kesi inayowahusu Mashahidi wa Yehova 16 huko Taganrog inakaribia kwisha. Kesi hiyo imeendeshwa kwa zaidi ya miaka miwili. Mashahidi wameshtakiwa kuwa wahalifu kwa sababu ya imani yao. Huenda baadhi yao watafungwa na kutozwa faini kubwa. Kuendeshwa kwa muda mrefu kwa kesi hiyo kumewaathirije Mashahidi hao? Itakuwaje ikiwa watashindwa kesi hiyo?