Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

UFARANSA

Maelezo Mafupi Kuhusu Ufaransa

Maelezo Mafupi Kuhusu Ufaransa

Mashahidi wa Yehova nchini Ufaransa walisajiliwa kisheria mwaka 1906, na kwa ujumla wanafurahia uhuru wa ibada. Hata hivyo, katikati ya miaka ya 1990 ripoti ya bunge yenye kichwa “Madhehebu nchini Ufaransa” iliwajumuisha Mashahidi wa Yehova katika orodha ya madhehebu yanayodaiwa kuwa hatari. Licha ya kutokuwa na athari yoyote kisheria, ripoti hiyo ilitumika kuchochea chuki na ubaguzi dhidi ya Mashahidi.

Shambulio la wazi kabisa lililowahi kutokea ni lile la serikali kupandisha kodi kupita kiasi ili makao kuu ya Mashahidi wa Yehova nchini humo yashindwe kujiendesha kiuchumi. Baada ya kuendesha kesi kwa muda wa miaka 16, hatimaye Juni 30, 2011, Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) ilitoa hukumu ya kukata maneno kwamba serikali ya Ufaransa ilikiuka uhuru wa ibada wa Mashahidi. Katika visa kadhaa Mashahidi wa Yehova nchini Ufaransa walikabili ubaguzi, walinyimwa usajili, hawakuruhusiwa kujenga majengo ya ibada na pia walizuiwa kukodi kumbi za manispaa ili kufanya shughuli za dini.

Ubaguzi wa serikali ya Ufaransa dhidi ya Mashahidi wa Yehova umesababisha waendelee kutiliwa shaka licha ya hukumu iliyotolewa na ECHR pamoja na ushindi mbalimbali katika mahakama za nchi hiyo. Matokeo ni kwamba, kuna matukio yanayoendelea ambapo Mashahidi hupigwa na kuteswa na majengo yao ya ibada kuharibiwa.