Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

TURKMENISTAN

Wamefungwa kwa Sababu ya Imani Yao

Wamefungwa kwa Sababu ya Imani Yao

Mnamo Machi 14, 2015, polisi jijini Turkmenabad walivamia mkutano wa kidini uliokuwa ukifanywa kwa amani kwenye nyumba ya Bahram Hemdemov. Mashahidi 38 walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kuendesha shughuli za dini kinyume cha sheria. Wote walitendewa kwa njia isiyofaa, 30 walitozwa faini, na wanane wakahukumiwa kifungo cha siku 15 gerezani. Hatimaye mahakama ya Mkoa ilimhukumu Bw. Hemdemov kifungo cha miaka minne gerezani. Kwa sasa amewekwa kizuizini kwenye kambi ya kazi ngumu ya Seydi. Mashahidi wa Yehova wanajitahidi kushughulikia kisa chake ili kumtoa katika kifungo hicho kisichozingatia haki.

Akamatwa kwa Mashtaka ya Uwongo

Mansur Masharipov, mwenye umri wa miaka 32 ni Shahidi ambaye alikamatwa Juni 30, 2016 na kuwekwa rumande na polisi ambao walikuwa wakimtafuta tangu mwaka 2014. Ingawa yeye ndiye aliyeshambuliwa vibaya na maofisa wa polisi, alishtakiwa kwa kumshambulia afisa wa polisi. Agosti 18, 2016, mahakama ya Turkmenistan ilimhukumu kifungo cha mwaka mmoja kwenye gereza la wahalifu. Bw. Masharipov amekata rufaa kutokana na hukumu hiyo.

Uhuru wa Dhamiri, Dini, na Imani Bado Hauzingatiwi

Mwaka 2015 na 2016, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu (CCPR) walitoa maamuzi tisa yaliyounga mkono malalamiko ya wanaume Mashahidi ambao walifungwa kwenye mazingira magumu kwa walikataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Kwa sasa nchi ya Turkmenistan haiwahukumu kifungo wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

Mashahidi wengine wawili waliofungwa kwa sababu ya mashtaka ya uwongo ambayo kwa wazi yalikusudiwa kuzuia utendaji wao wa dini, wao pia walipeleka malalamiko yao CCPR. Katika maelezo ya Baraza hilo yanayohusu suala la haki za kibinadamu nchini Turkmenistan yaliyotolewa Aprili 2012, liliiomba serikali “ihakikishe kwamba sheria na utendaji unaohusiana na usajili wa mashirika ya kidini unazingatia haki ya watu ya kufuata na kuonyesha wazi imani yao ya kidini kwa mujibu wa Mkataba [Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa].” Mashahidi walipeleka maombi ya kusajiliwa kisheria mwaka 2008, lakini serikali ilikataa kuwasajili kisheria.

Matarajio ya Mabadiliko

Mashahidi wa Yehova wanafurahi kuona kwamba serikali ya Turkmenistan imewaachilia huru Mashahidi waliofungwa ili kuondoa ukosefu wa haki. * Wanatarajia kwamba serikali itachukua hatua zinazofaa kama maamuzi ya CCPR yanavyoonyesha—kuheshimu kabisa haki za binadamu na hasa haki ya uhuru wa dhamiri, dini na imani. Wakili mmoja wa Mashahidi wa Yehova alisema hivi: “Mashahidi wa Yehova wanatarajia kwamba wataafikiana na serikali ya Turkmenistan na kutatatua mahangaiko ya serikali kwa njia ambayo itaruhusu Mashahidi kubaki wakiwa na dhamiri safi na amani katika ujitoaji wao kwa Mungu.”

Mfuatano wa Matukio

 1. Agosti 18, 2016

  Mansur Masharipov alifunguliwa mashtaka ya uwongo na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani.

 2. Julai 2016

  CCPR ilitoa maamuzi matano yaliyowaunga mkono Mashahidi ambao walikuwa wameteswa kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 3. Desemba 14, 2015

  CCPR ilitoa maamuzi yaliyowaunga mkono Mashahidi watatu ambao waliteswa kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Uamuzi mwingine uliowaunga mkono Mashahidi ulitolewa Mei 19, 2015.

 4. Mei 19, 2015

  Bahram Hemdemov atiwa hatiani kwa kufanya shughuli za dini na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne jela. Miezi miwili kabla ya hukumu alikamatwa kabla ya kuwekwa mahabusu.

 5. Februari/Machi 2015

  Mashahidi wawili waliofungwa kwa kukataa utumishi wa jeshi kwa sababu ya dhamiri waachiliwa huru.

 6. Novemba 18, 2014

  Jumla ya Mashahidi wawili wafungwa kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri.

 7. Oktoba 22, 2014

  Rais wa Turkmenistan atoa msamaha na kuwaachilia huru Mashahidi nane wa Yehova.

 8. Septemba 30, 2014

  Mashahidi tisa wafungwa—saba kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri na kama adhabu, wawili washtakiwa mashtaka ya uwongo kwa sababu ya utendaji wa kidini.

 9. Septemba 2, 2014

  Wenye mamlaka nchini Turkmenistan wamwachilia Bibi Rahmanova na wabadili adhabu yake ya kifungo cha miaka minne gerezani kuwa kifungo chenye masharti, nje ya gereza.

 10. Agosti 18, 2014

  Bibi Rahmanova ashtakiwa kwa mashtaka ya uwongo na kuhukumiwa miaka minne gerezani.

 11. Julai 25, 2014

  Mashahidi saba wako gerezani—watano kwa mashtaka ya kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri na wawili kwa mashtaka ya uwongo kwa sababu ya utendaji wao wa kidini.

 12. Aprili 6, 2014

  Mashahidi 26 wawekwa kizuizini, 13 kati yao walikamatwa bila ushahidi wa kosa lolote. Mashahidi hao 13 walihukumiwa kulipa faini.

 13. Novemba 2013

  Mashahidi tisa bado wako gerezani—nane kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri na mmoja kwa mashtaka ya uwongo yanayohusiana na utendaji wa kidini.

 14. Agosti 29, 2013

  Mashahidi watatu wapeleka malalamiko yao kwenye kamati ya CCPR kutokana na serikali ya Turkmenistan kushindwa kutambua haki yao ya kutojiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 15. Mei 1, 2013

  Mashahidi wawili wapeleka malalamiko yao kwenye kamati ya CCPR kutokana na serikali ya Turkmenistan kushindwa kutambua haki yao ya kutojiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 16. Januari 24, 2013

  Maofisa 30 wa polisi wavamia nyumba ya Navruz Nasyrlaye majuma matatu tu baada ya CCPR kulalamikia serikali ya Turkmenistan. Polisi waliwapiga sana watu wa familia hiyo na wageni wao waliokuwepo.

 17. Septemba 7, 2012

  Mashahidi 10 wapeleka malalamiko yao kwenye kamati ya CCPR kutokana na serikali ya Turkmenistan kukataa kutambua haki yao ya kutojiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Navruz Nasyrlayev ndiye mlalamikaji mkuu.

 18. Agosti 21, 2008

  Mashahidi wa Yehova wapeleka ombi la kutaka kusajiliwa nchini Turkmenistan.