Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

SEPTEMBA 14, 2016
TURKMENISTAN

Wenye Mamlaka Jijini Ashgabad Wamfunga Mansur Masharipov kwa Mashtaka ya Uwongo

Wenye Mamlaka Jijini Ashgabad Wamfunga Mansur Masharipov kwa Mashtaka ya Uwongo

Juni 30, 2016, maofisa wa serikali walimkamata Mansur Masharipov, kwenye eneo la umma la jiji la Ashgabad, Turkmenistan. Polisi walikuwa wakimtafuta tangu mwaka wa 2014 kwa sababu ya shughuli zake za kidini akiwa Shahidi wa Yehova. Bw. Masharipov, mwenye umri wa miaka 32, alishtakiwa kwa kosa la kumshambulia ofisa wa polisi, ingawa yeye ndiye aliyeshambuliwa na maofisa wa polisi waliomtendea kikatili. Hii si mara ya kwanza kwa Bw. Masharipov kutendewa vibaya na hata kuteswa kwa sababu ya shughuli za kidini anazofanya kwa amani. Agosti 18, 2016, mahakama ya Turkmenistan ilimhukumu Bw. Masharipov kifungo cha mwaka mmoja gerezani. Amekata rufaa kupinga hukumu hiyo.