Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Bahram na mke wake, Gulzira

OKTOBA 24, 2016
TURKMENISTAN

Je, Bahram Hemdemov Ataachiliwa Huru Msamaha wa Wafungwa Utakapotolewa Tena?

Je, Bahram Hemdemov Ataachiliwa Huru Msamaha wa Wafungwa Utakapotolewa Tena?

Mnamo Februari 2016, serikali ya Turkmenistan ilitangaza msamaha na kuwaachilia huru mamia ya wafungwa lakini haikumwachilia huru Bahram Hemdemov. Karibu miezi mitatu hivi baadaye Mahakama Kuu ya Turkmenistan ilikataa kusikiliza rufani yake aliyoiwasilisha kupinga mashtaka na kifungo alichohukumiwa. Agosti 15, 2016, wakili wa Bw. Hemdemov alifungua kesi kwenye Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu kwa niaba ya Bw. Hemdemov.

Mateso ya Mashahidi wa Yehova Jijini Turkmenabad

Siku ambayo Bw. Hemdemov alikamatwa mnamo Machi 2015, alikuwa kwenye mkutano wa dini pamoja na Mashahidi wenzake uliofanywa kwa amani kwenye nyumba yake iliyopo jijini Turkmenabad. Maofisa wa polisi walifika bila kibali cha upekuzi, wakavamia na kupekua nyumba yake, wakachukua mali zake za kibinafsi, na kuwatendea isivyo haki watu wote waliohudhuria.

Wakili wa Bw. Hemdemov alisema hivi: “Polisi waliamua kumtesa sana Bahram Hemdemov ili kuwaogopesha Mashahidi wengine wanaoishi jijini Turkmenabad.” Licha ya mateso hayo kutoka kwa wenye mamlaka, Bw. Hemdemov bado anaendelea kushika imani yake.

Matarajio ya Kuachiliwa

Mashahidi wa Yehova wanatarajia kwamba hivi karibuni serikali ya Turkmenistan itamwachilia huru Bw. Hemdemov kutoka gerezani. Itakuwa ishara ya fadhili kwa Rais Gurbanguly Berdimuhamedov kumwachilia huru Bw. Hemdemov atakapotoa tena msamaha kwa wafungwa.

Mke wa Bw. Hemdemov, anayeitwa Gulzira, watoto wao wanne, na pia Mashahidi wenzake wanamkosa sana, wangependa arudi nyumbani. Mashahidi nchini Turkmenistan wanaiomba serikali iwaruhusu kuabudu pamoja kwa amani, bila kuingiliwa na wenye mamlaka.