Turkmenistan
Turkmenistan Imepuuza Haki ya Uhuru wa Dhamiri
Mashahidi wawili wa Yehova wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kukataa kujiunga na utumishi wa kijeshi. Mpaka sasa Turkmenistan bado haitambui haki ya msingi ya wanaokataa kujiunga na utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri na haina mpango wa utumishi wa badala wa kiraia.
Je, Turkmenistan Itatekeleza Uamuzi wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu?
Serikali ya Turkmenistan imeagizwa iheshimu mikataba yake ya kulinda haki za kibinadamu, kutia ndani uhuru wa mawazo, dhamiri na ibada.