Mashahidi wa Yehova wamekuwepo nchini Namibia tangu 1929. Hata hivyo, serikali ya Afrika Kusini, iliyotawala Namibia kwa amri ya Ushirika wa Mataifa, ilidhibiti utendaji wao. Tangu miaka ya 1950 hadi mwishoni mwa miaka ya 1970, wenye mamlaka hawakuwaruhusu watu weupe kuingia katika maeneo ya watu weusi bila kibali cha serikali na hivyo utendaji wa wamishonari kutoka nje ya nchi ulikuwa mdogo. Katika miaka hiyo, Mashahidi walikabili upinzani mkali kutoka kwa viongozi wa kidini na wenye mamlaka kwa sababu ya kushiriki imani yao ya kidini na wengine.

Machi 21, 1990, Namibia ilipata uhuru kutoka kwa Afrika Kusini. Chini ya katiba mpya, Mashahidi wa Yehova walipata uhuru mwingi zaidi wa kufanya utendaji wao wa kidini. Katika mwaka wa 2008, wakasajiliwa kisheria. Mashahidi wa Yehova nchini Namibia wanathamini sana kuwa na uhuru wa kuabudu.