Karibuni Mahakama Kuu ya Kyrgyzstan itasikiliza kesi mbili zinazohusu haki ya uhuru wa kidini, kushirikiana, na kusema.

  • Februari 15, 2016. Mashahidi wa Yehova walikata rufani uamuzi wa Kamati ya Mambo ya Dini uliokataa kutoa usajili kwa mashirika manne ya kidini. Uamuzi wa kamati hiyo unapuuza maamuzi ya Septemba 4, 2014, ya Baraza la Katiba kuhusu usajili.

  • Februari 24, 2016. Mwendesha-mashtaka wa jiji la Osh alikata rufani uamuzi wa mahakama za mwanzo ya kuwaachilia huru Oksana Koriakina na mama yake, Nadezhda Sergienko. Mashahidi wa Yehova wamesikitishwa na uamuzi wa Ofisi ya Mwendesha-Mashtaka Mkuu wa kuwasilisha kesi hiyo mahakamani kwa niaba ya Ofisi ya Mwendesha-Mashtaka wa Jiji la Osh, kwa kuwa hukumu za awali za mahakama za mwanzo zinaonyesha wazi kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za kikatiba.