Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JULAI 2, 2015
KOREA KUSINI

Wafungwa wa Muda Mrefu—Je, Watapata Uhuru?

Wafungwa wa Muda Mrefu—Je, Watapata Uhuru?

Katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, Korea Kusini imewahukumu vijana zaidi ya 18,000 kifungo cha jumla ya miaka 35,000 kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Maoni ya watu kuhusu jambo hili yanabadilika jinsi gani nchini Korea Kusini? Je, utafika wakati ambapo watu watakuwa huru kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri zao nchini humo? Jamii za kimataifa zina maoni gani kuhusu kutojiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri? Video hii inaonyesha changamoto zinazofanya Korea Kusini ishindwe kutatua hali hiyo.