Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

KOREA KUSINI

Wamefungwa kwa Sababu ya Imani Yao

Wamefungwa kwa Sababu ya Imani Yao

Mashahidi wa Yehova wamekuwapo nchini Korea Kusini kwa zaidi ya miaka 100 na wamekuwa wakifurahia uhuru wa ibada—isipokuwa wale wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Kila mwaka, serikali ya Korea Kusini huwafunga gerezani wanaume wengi vijana ambao ni Mashahidi. Tangu enzi ya Vita vya Korea hadi leo, Korea Kusini imeendelea kuwashtaki bila huruma wanaume vijana Mashahidi wanaokataa kujiunga na jeshi, na serikali haijaandaa utumishi wa badala wa kiraia ili kusuluhisha tatizo hilo. Matokeo ni kwamba Korea Kusini imewahukumu na kuwafunga Mashahidi zaidi ya 18,000 kwa jumla ya miaka 36,000 kwa sababu ya kukataa kujiunga na jeshi.

Maoni ya Shirika la Kimataifa Kuhusu Haki ya Kukataa Kujiunga na Jeshi kwa Sababu ya Dhamiri

Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (CCPR), ambayo hufuatilia kutekelezwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR), imesema tena na tena kwamba Korea Kusini * inakiuka haki za watu wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri inapowahukumu na kuwafunga gerezani.Hivi karibuni, mwezi wa Januari 14, 2015, CCPR ilitoa uamuzi wake wa tano dhidi ya Korea Kusini kuhusiana na jambo hili. Uamuzi huo unaohusisha Mashahidi 50 waliokuwa wamefungwa, uliunga mkono uamuzi wa mapema ulioeleza kwamba serikali ya Korea Kusini ilikuwa imekiuka haki ya Mashahidi ya “uhuru wa kufikiri, dhamiri na dini.“ Pia, CCPR ilieleza kuwa serikali hiyo ilikuwa na hatia ya kutoa “vifungo visivyo na misingi ya kisheria“ kwa kuwaadhibu wanaume hao vifungo vya gerezani kwa kutumia haki iliyotolewa na ICCPR.

Baada ya kuchunguza rekodi yote ya haki za kibinadamu ya Korea Kusini, CCPR ikatoa maoni yake Novemba 3, 2015. Iliisihi serikali ya Korea Kusini kuwaachilia huru wote walio gerezani kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri, kufuta rekodi yao ya uhalifu na kuwalipa fidia, na kuweka sheria inayoruhusu utumishi badala wa kiraia. Pia lieleza kwamba serikali “inapaswa kutekeleza kikamili Maamuzi ambayo [CCPR] imetoa kufikia sasa.”

Maoni ya Watu Nchini Korea Kusini

Serikali inashinikizwa kutoka ndani ya nchi kuweka sheria inayoruhusu programu inayokubalika ya utumishi badala wa kiraia kwa wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Mahakimu wa mahakama ya Wilaya wamewatangaza Mashahidi tisa waliokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri kuwa “hawana hatia.” Baadhi ya mahakama za wilaya zimepeleka kesi zisikilizwe kwenye Mahakama ya Kikatiba. Julai 9, 2015, Mahakama hiyo ilijadili ikiwa kukataa kwa serikali kutambua haki ya wanoakataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri ni kinyume cha katiba. Mwaka 2004 na 2011 Mahakama hiyo ya Kikatiba ilitoa umuzi kwamba kitendo cha Sheria ya Utumishi wa Jeshi kutowatambua wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri si kinyume cha katiba. Tunasubiri uamuzi mpya wa mahakama hiyo.

Mfululizo wa Matukio

 1. Aprili 30, 2017

  Jumla ya Mashahidi wa Yehova 401 watumikia vifungo gerezani kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 2. Novemba 3, 2015

  CCCPR yatoa uamuzi wake, na kuisihi Korea Kusini kuanza programu ya utumisha badala wa kiraia.

 3. Julai 9, 2015

  Mahakama ya Kikatiba yajadili ikiwa vipengele fulani vya Sheria ya Utumishi wa Jeshi vinapatana na katiba.

 4. Januari 14, 2015

  CCPR ilitoa Uamuzi kwamba Korea Kusini imekiuka Kifungu cha 18 (haki ya uhuru wa kufikiri, dhamiri, na wa kidini) na Kifungu cha 9 (kinachokataza kuwafunga watu bila misingi ya kisheria) cha ICCPR kwa kuwanyima Mashahidi 50 haki yao ya kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri na kuwafunga gerezani.

 5. Juni 30, 2014

  Kesi 28 zinazohusiana na kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri bado ziko kwenye Mahakama ya Kikatiba; wanaume 618 wafungwa gerezani.

 6. Januari 28, 2014

  Rais atoa msamaha wa pekee ili washtakiwa waachiliwe kwa dhamana na kupunguza kwa mwezi mmoja au miwili vifungo vya gerezani vya wanaume Mashahidi 100 hivi waliozuiliwa kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri; 513 wafungwa gerezani kufikia Januari 31.

 7. Novemba 2013

  Jumla ya Mashahidi 599 wakamatwa kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 8. Aprili 2013

  Asilimia 70 ya Mashahidi watenganishwa na wafungwa wengine na kuwekwa katika vyumba vya Mashahidi wenzao.

 9. Oktoba 25, 2012

  CCPR yaunga mkono Uamuzi wa kwamba Korea Kusini ilikiuka Kifungu cha 18 (haki ya uhuru wa kufikiri, dhamiri na dini) cha ICCPR kwa kuwanyima Mashahidi 388 haki ya kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 10. Agosti 30, 2011

  Mahakama ya Kikatiba yaamua kwamba sheria ya kuwashtaki na kuwahukumu watu wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri haivunji katiba ya Korea Kusini.

 11. Machi 24, 2011

  CCPR inakubaliana na Uamuzi wa kwamba Korea Kusini ina hatia ya kuvunja Kifungu cha 18 cha mkataba wa ICCPR kwa kuwanyima Mashahidi 100 haki ya kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 12. Januari 15, 2009

  Tume ya Rais ya Kuchunguza Vifo Visivyo vya Kawaida Katika Jeshi inatoa ripoti inayothibitisha kwamba serikali ya Korea Kusini ilihusika katika vifo vya Mashahidi vijana watano kuanzia mwaka wa 1975 hadi 1985 waliofungwa gerezani kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 13. Desemba 2008

  Korea Kusini yafutilia mbali mipango ya kuanzisha utumishi wa badala wa kiraia kwa ajili ya watu wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 14. Septemba 18, 2007

  Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini yatangaza mpango wa kuwaruhusu watu wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri kwa msingi wa kidini wafanye utumishi wa badala wa kiraia, na kuahidi kurekebisha sheria ya utumishi wa kijeshi na sheria ya jeshi la akiba.

 15. Novemba 3, 2006

  CCPR inaunga mkono Uamuzi wa kwamba Korea kusini ina hatia ya kuvunja kifungu cha 18 cha mkataba wa ICCPR kwa kuwanyima Mashahidi wawili haki ya kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 16. Agosti 26, 2004

  Mahakama ya Kikatiba yaunga mkono wazo la kwamba sheria ya kuwaadhibu watu wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri inapatana na katiba.

 17. 2001

  Mamlaka ya Kusimamia Wanajeshi yaacha kuwalazimisha watu kujiandikisha jeshini, na urefu wa vifungo vya gereza unapunguzwa kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja na nusu.

 18. Desemba 1, 1985

  Kim, Young-geun afa kutokana na kuteswa kinyama na wanajeshi alipofungwa gerezani kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 19. Agosti 17, 1981

  Kim, Sun-tae afa kutokana na kutendewa kinyama na wanajeshi alipofungwa kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 20. Machi 28, 1976

  Jeong, Sang-bok afa kutokana na kupigwa vibaya na kutendewa kikatili kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 21. Machi 19, 1976

  Lee, Choon-gil afa baada ya wengu kupasuka kutokana na kupigwa vibaya na askari-jeshi alipofungwa gerezani kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 22. Novemba 14, 1975

  Kim, Jong-sik afa baada ya kupigwa vibaya na kuteswa na askari-jeshi kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

 23. 1975

  Rais Park Jeong-Hee aanzisha sheria kali ya kuwalazimisha watu kujiandikisha jeshini, akiamuru watu wote kutii kikamili amri hiyo. Wanaume Mashahidi wapelekwa kwa lazima kwenye vituo vya kuandikisha wanajeshi.

 24. Januari 30, 1973

  Kuanza kutekelezwa kwa Sheria Maalumu ya Kuwaadhibu Kama Wahalifu Watu Wanaovunja Sheria ya Utumishi wa Kijeshi, jambo lililoongeza urefu wa vifungo vya gerezani kutoka miaka mitatu hadi kumi kwa wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Wengi walazimishwa tena na tena kujiandikisha jeshini.

 25. 1953

  Wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri waanza kufungwa gerezani nchini Korea Kusini.

^ fu. 4 Korea Kusini ilitia sahihi Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) na ni mojawapo ya nchi zilizotia sahihi mkataba wa kwanza wa ziada wa ICCPR unaowawezesha watu mmoja-mmoja nchini Korea Kusini kuiandikia CCPR wakilalamikia kuvunjwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa.