Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

MAMBO YA KISHERIA NA HAKI ZA KIBINADAMU

Mambo ya Kisheria Nchini Korea Kusini

JANUARI 25, 2017

“Mahakama Yatoa Uamuzi Bora wa Mwaka”

Mahakama ya Rufani ya Gwangju imetoa uamuzi wa “kutokuwa na hatia” kwa vijana watatu waliokataa kujiunga na utumishi wa kijeshi. Nchi nzima inasubiri mahakama kuu itoe uamuzi wake.

JANUARI 25, 2017

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kitaifa Yasihi Uhuru wa Dhamiri Uheshimiwe

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Korea Kusini yaisihi serikali kulinda haki ya msingi ya wale wanaokataa kujiunga na utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri.

DESEMBA 20, 2016

Mahakama ya Kikatiba ya Korea Kusini Itatoa Uamuzi Muhimu Hivi Karibuni

Ikiwa uamuzi wa Mahakama utawaunga mkono wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri, utaimarisha haki ya uhuru wa dhamiri na dini kwa raia wote wa Korea Kusini.