Hamia kwenye habari

DESEMBA 21, 2017
KAZAKHSTAN

Mahakama Kuu ya Kazakhstan Imekataa Rufaa ya Teymur Akhmedov

Mahakama Kuu ya Kazakhstan Imekataa Rufaa ya Teymur Akhmedov

Desemba 4, 2017, Mahakama Kuu ya Kazakhstan ilitupilia mbali rufaa ya Teymur Akhmedov ya kupinga kushtakiwa isivyo haki kwa madai ya kushiriki utendaji wa kidini kinyume cha sheria. Ukweli ni kwamba alikuwa tu akiwaeleza wengine kuhusu imani yake ya kidini. Bw. Akhmedov amefungwa tangu alipokamatwa Januari 18, 2017, kwa kuhusishwa katika kesi ambayo ilitayarishwa kama mtego na askari wa siri. Mwezi Mei alishtakiwa katika mahakama ya wilaya na akahukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani, hukumu ambayo iliungwa mkono na mahakama ya rufaa Juni 20, 2017.

Ilipochunguza rufaa yake, Mahakama kuu ilipuuza uamuzi wa hivi karibuni wa Kamati ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Vifungo Visivyo vya Haki, ambayo ilisema kwamba Kazakhstan ina hatia ya kumfunga isivyo haki Bw. Akhmedov na kukiuka uhuru wake wa ibada. Licha ya kuwa na afya mbaya, Bw. Akhmedov anadumisha imani yenye nguvu na anamtegemea Mungu kikamili. Bw. Akhmedov anashukuru kwa jitihada kubwa zinazofanywa ili aweze kutoka mapema gerezani, hata ingawa kufikia sasa jitihada hizo hazijafanikiwa na anashukuru kwamba waabudu wenzake ulimwengu pote wanaendelea kusali kwa ajili yake ili aweze kuachiliwa mapema.