Mambo ya Kisheria Nchini Kazakhstan
Teymur Akhmedov Ameachiliwa kwa Msamaha wa Rais
Rais wa Kazakhstan Nursultan Nazarbayev amempa msamaha Teymur Akhmedov, ambaye alikuwa amefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kuwaeleza wengine kuhusu imani yake ya dini. Msamaha huo umefuta rekodi yake ya uhalifu.