Hamia kwenye habari

JANUARI 30, 2017
ERITREA

Shahidi Mwingine Nchini Eritrea Amekufa Baada ya Kutoka Gerezani

Shahidi Mwingine Nchini Eritrea Amekufa Baada ya Kutoka Gerezani

Tsehaye Tesfamariam alikufa akiwa Asmara Novemba 30, 2016. Aliachiliwa kutoka gerezani Septemba 10, 2015, kwa sababu alikuwa akiumwa sana na hakupata huduma inayofaa ya afya wala matibabu alipokuwa kifungoni. Tsehaye Tesfamariam alizaliwa mwaka wa 1941 jijini Nefasit, Eritrea. Ameacha mke, Hagosa Kebreab, ambaye alimwoa mwaka wa 1973 na mabinti wanne na wavulana watatu. Alibatizwa na kuwa Shahidi wa Yehova mwaka wa 1958.

Bw. Tesfamariam alikuwa amefungwa katika Kambi ya Meitir tangu alipokamatwa bila sababu yoyote mnamo Januari 2009. Oktoba 5, 2011, Bw. Tesfamariam na wanaume wengine 24 ambao ni Mashahidi walifungwa katika Kambi ya Meitir kwenye jengo la chuma ambalo nusu ya jengo hilo limefukiwa chini ya ardhi kwa ajili ya adhabu maalumu. Walikaa ndani ya jengo hilo mpaka Agosti 2012. Baada ya kuvumilia joto kali, chakula kidogo, na maji machache waliyopewa, afya yao ilikuwa mbaya sana.

Matokeo ni kwamba wafungwa Misghina Gebretinsae na Yohannes Haile walikufa wakiwa katika gereza hilo la Meitir, na Kahssay Mekonnen na Goitom Gebrekristos walikufa baada ya kuachiliwa kutoka gerezani. Kifo cha Bw. Tesfamariam kinaongeza idadi ya wafungwa waliokufa.