Baada ya kukaa miezi 11 gerezani, Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova waliachiliwa Januari 28, 2016. Hakimu Akram Gahramanov alikuwa amewafunga na kudai walipe faini kubwa sana (manat 7,000 , au euro 3,932) kwa kuwaachia watu broshua moja ya kidini. Kwa kuwa wanawake hao wamekaa gerezani tangu Februari 17, 2015 aliamua kufuta faini zao. Uamuzi huo unakiuka uamuzi wa Umoja wa Mataifa ulioagiza kwamba Serikali ya Azerbaijan iwalipe fidia wanawake hao kwa kuwafunga kinyume cha sheria.

Ingawa afya yao ni mbaya, Bi. Zakharchenko na Bi. Jabrayilova wamefurahi kuwa huru. Sasa wako nyumbani pamoja na familia zao na wanaendelea kupata nafuu.