Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

MACHI 7, 2016
AZERBAIJAN

Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova Wakata Rufani kwa Kuhukumiwa Kuwa na Hatia

Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova Wakata Rufani kwa Kuhukumiwa Kuwa na Hatia

Machi 9, 2016, Mahakama ya Rufaa ya Baku itasikiliza malalamiko ya Zakharchenko na Valida Jabrayilova kuhusu jinsi walivyohukumiwa kinyume cha sheria kwa sababu ya kusambaza machapisho ya kidini. Wanawake hao wanataka hukumu hiyo ifutwe, walipwe gharama zote walizotumia kuendesha kesi hiyo, na walipwe fidia kwa ukiukwaji wa haki zao walipokuwa kifungoni kwa karibu mwaka mmoja.

Mapema kikundi cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia vifungo vilivyo kinyume cha sheria kilitoa Uamuzi wao rasmi uliobainisha kwamba wenye mamlaka nchini Azerbaijan walikuwa wamekiuka haki za Bi. Zakharchenko na Bi. Jabrayilova na kwamba walistahili kulipwa fidia kwa kutendewa kinyume cha haki. Mahakama ilipotoa hukumu yake Januari 28, 2016, ilipuuza uamuzi huo na kuwahukumu kuwa na hatia wanawake hao.