Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

MEI 19, 2015
AZERBAIJAN

Azerbaijan Yaongezea Muda wa Vifungo Visivyo na Msingi vya Wanawake Wawili

Azerbaijan Yaongezea Muda wa Vifungo Visivyo na Msingi vya Wanawake Wawili

Wizara ya Usalama wa Taifa ya Azerbaijan imeongeza muda wa vifungo vya Mashahidi wawili wa Yehova, Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova . Februari 17, 2015, Wizara hiyo (MNS) iliwasilisha mashtaka ya uhalifu wa kusambaza machapisho ya Biblia bila “ruhusu” na kuwafunga wanawake hao. Mei 7, 2015, Mahakama ya Wilaya ya Sabail ilikubali kuwafunga hadi Julai 17. Mahakama imekataa maombi ya kubadili kifungo hicho kiwe kifungo cha nyumbani. Mawakili wa Mashahidi hao wamekata rufani kupinga vifungo hivyo visivyo vya haki na wameeleza hangaiko lao kuhusu hali ya kiakili, kihisia, na kimwili ya wanawake hao. Wenye mamlaka wanaendelea kuwafanyia uchunguzi Mashahidi wengine.