Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

AZERBAIJAN

Wafungwa kwa Sababu ya Imani Yao

Wafungwa kwa Sababu ya Imani Yao

Serikali ya Azerbaijan inaendelea kuwaadhibu Mashahidi ya Yehova kwa kufanya ibada yao. Mahakama zinawahukumu kama wahalifu kwa sababu ya kukutana pamoja kwa ibada, kuzungumza na wengine kuhusu imani yao, na kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri. Mahakimu hao huwatoza faini kubwa na kuwafunga gerezani.

Wanawake Wawili Wafungwa kwa Kuhubiri

Desemba 17, 2015, kesi ya Mashahidi wawili wa Yehova, Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova, ilianza kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Pirallahi jijini Baku. Bi. Zakharchenko na Bi. Jabrayilova wamefungwa gerezani tangu Februari 17, 2015, kwa shtaka la kusambaza machapisho ya kidini bila “ruhusa maalumu.”

Wanawake hao wameathirika kiafya na kihisia baada ya kufungwa gerezani kwa miezi kumi sasa. Hata hivyo, walipokuwa mahakamani kwa mara ya kwanza kabla ya kesi kuanza kusikilizwa, hakimu alikataa maombi yote na alikataa kubadili kifungo chao kiwe kifungo cha nyumbani. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Januari 7, 2016.

Azerbaijan Yashindwa Kutimiza Matakwa

Katika ripoti yake ya mwaka wa 2011 ya kuchunguza nchi ya Azerbaijan, Tume ya Ulaya Inayopinga Ubaguzi wa Kidini na wa Kijamii (ECRI) ya Baraza la Ulaya iliisihi mara kadhaa serikali ya Azerbaijan ihakikishe kwamba “sheria iliyopo . . . inaheshimu kabisa uhuru wa kidini kupatana na viwango vya Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu.” Mnamo 2012, Tume ya Venice ya Baraza la Ulaya ilichapisha mapendekezo ya kina kuhusu mabadiliko ambayo nchi ya Azerbaijan inapaswa kufanya katika Sheria Kuhusu Uhuru wa Imani ya Kidini. Tume hiyo ilisema: “Sheria hiyo ina vipengele kadhaa ambavyo vinaenda kinyume na viwango vilivyopo vya kimataifa. . . . Baadhi ya mambo muhimu ya kisheria yanayohitaji kusuluhishwa ni kama vile upana wa sheria yenyewe na uhuru wa kidini na wa dhamiri wa wananchi, masuala ya usajili, masuala yanayohusu uhuru na vizuizi vya mashirika ya kidini; kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri, suala la kuwashawishi watu wabadili imani yao, na kuchapisha na kusambaza machapisho ya kidini.”

Azerbaijan imekataa pia kuheshimu haki ya watu ya kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri. Kama takwa la kujiunga na Baraza la Ulaya katika mwaka wa 1996, Azerbaijan ilikubali (1) kutunga sheria ya utumishi wa kiraia wa badala ndani ya miaka miwili ya kuanza kutawala, (2) kufutilia mbali mashtaka ya wote waliofungwa kwa sababu ya kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri, na (3) kuwaruhusu wanaokataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri kufanya utumishi wa badala wa kiraia. Zaidi ya miaka 13 baada ya kujiunga na Baraza la Ulaya, bado Azerbaijan haijatimiza takwa hilo.

Ripoti hiyo ya Mei 2011 ilisema hivi: “ECRI inaihimiza serikali ya Azerbaijan kutunga sheria haraka ya kukubali utumishi wa badala wa kiraia kupatana na viwango vya Ulaya. . . . [ECRI] inarudia kwa kukazia pendekezo lake kwamba serikali haipaswi kuwashtaki na kuwafunga wanaokataa utumishi wa kijeshi badala yake wanapaswa kupewa nafasi ya kufanya utumishi mwingine kwa jamii unaopatana na dhamiri yao.”

Je, Azerbaijan Itatekeleza Dai Lake la Kukubali Uhuru wa Kidini?

Juni 25, 2015, Tume ya Marekani Kuhusu Helsinki ilieleza kwamba ina wasiwasi kuhusu “kuongezeka kwa mkazo hivi karibuni dhidi ya dini zenye watu wachache—hasa Mashahidi wa Yehova—nchini Azerbaijan.” Mwenyekiti wa tume hiyo, Mjumbe Chris Smith, alisema hivi: “Mara nyingi Serikali hiyo hujisifu kwamba ina rekodi nzuri ya kulinda uhuru wa kidini lakini ukweli ni kwamba imewafunga watu wengi sana kwa sababu ya imani yao. Ninaisihi Serikali ya Azerbaijan imwachilie Bi. Zacharchenko na Bi. Jabrayilova mara moja.”

Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote wameeleza wazi hangaiko lao kuhusu hali ya Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova. Kamati ya Umoja wa Maifa ya Haki za Kibinadamu ilitoa ombi rasmi kwamba Bi. Zakharchenko atolewe gerezani na kupewa kifungo cha nyumbani, lakini mahakama ilipuuza ombi hilo. Bi. Zakharchenko na Bi. Jabrayilova pamoja na familia na marafiki wao wanaomba kwa heshima kwamba serikali ya Azerbaijan iwaachilie na kuwaondolea mashtaka mara moja.

Time Line

 1. Desemba 17, 2015

  Mahakama ya Wilaya ya Pirallahi jijini Baku inakataa maombi ya kumwachilia Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova kutoka gerezani. Kesi hiyo imepangwa kusikizwa tena Januari 7, 2016.

 2. Septemba 4, 2015

  Mahakama ya Wilaya ya Sabail jijini Baku inaendelea kumzuilia Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova bila kusikiliza kesi yao hadi Desemba 17, 2015, na hivyo kuwafunga kwa miezi kumi.

 3. Mei 7, 2015, na Julai 4, 2015

  Mahakama ya Wilaya Sabail jijini Baku inaendelea kumzuilia Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova bila kusikiliza kesi yao.

 4. Februari 17, 2015

  Mahakama ya Wilaya Sabail jijini Baku inaagiza kwamba Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova wafungwe mara moja kwa miezi mitatu kabla ya kesi yao kusikilizwa kwa shtaka la uhalifu la kugawa machapisho ya kidini.

 5. Marchi 12, 2013

  Kamran Mirzayev, mmoja wa Mashahidi wa Yehova, ashtakiwa na kuhukumiwa kifungo cha miezi tisa kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri. Baadaye, alipokuwa anatumikia kifungo chake, aliachiliwa kutoka gerezani kabla ya kumaliza kifungo chake kwa sababu ya msamaha wa serikali.

 6. Septemba 25, 2012

  Fakhraddin Mirzayev, one of Jehovah’s Witnesses, is convicted and given a one-year sentence for his conscientious objection to military service.

 7. Septemba 8, 2010

  Fakhraddin Mirzayev, mmoja wa Mashahidi wa Yehova, ashtakiwa na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri.

 8. Agosti 19, 2009

  Mushfig Mammedov akamatwa tena kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri, afungwa kabla ya kupelekwa mahakama, na kutozwa faini aliposhtakiwa mara ya pili.

 9. Marchi 7, 2008

  Wakili wa Mushfig Mammedov na wa Samir Huseynov wafungua mashtaka dhidi ya Serikali ya Azerbaijan kwenye Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu kwa kuwahukumu kuwa wahalifu kwa sababu ya kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri.

 10. Octoba 4, 2007

  Samir Huseynov, mmoja wa Mashahidi wa Yehova, afungwa gerezani na kuhukumiwa kifungo cha miezi kumi kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri.

 11. 2006

  Mushfig Mammedov, mmoja wa Mashahidi wa Yehova, afungwa kabla ya kupelekwa mahakamani, ashtakiwa kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri, na kuhukumiwa miezi sita hadi atakapokubali kufanya hivyo.