Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JANUARI 15, 2016
AZERBAIJAN

Hakimu Aahirisha Tena Kusikiliza Kesi na Kuchelewa Kuwaweka Huru Wanawake

Hakimu Aahirisha Tena Kusikiliza Kesi na Kuchelewa Kuwaweka Huru Wanawake

Januari 14, 2016, Hakimu Akram Gahramanov wa Mahakama ya Wilaya ya Pirallahi jijini Baku, Azerbaijan, ameahirisha tena kusikiliza kesi ya Bi. Zakharchenko na Bi. Jabrayilova. Alitoa sababu kwamba asingeweza kusikiliza kesi bila Bi. Zakharchenko kuwapo, ambaye afya yake haikumruhusu kufika mahakamani. Amepanga tena kusikiliza kesi Januari 28, 2016.

Kuchelewa kusikiliza kesi kunawaathiri wanawake hao, kwa sababu kunawanyima mawakili wao nafasi ya kuwatetea ili wawekwe huru. Kwa kuwa afya zao zimezorota kutokana na kufungwa kwa miezi 11, madai yasiyo na msingi ya kwamba lazima Bi. Zakharchenko afike mahakamani na pia kucheleweshwa kwa kesi yao, kunawaongezea wanawake hao mateso.