Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

JULAI 14, 2015
AZERBAIJAN

Azerbaijan Yaongeza Muda wa Miezi Miwili Zaidi wa Kifungo Kisicho na Haki

Azerbaijan Yaongeza Muda wa Miezi Miwili Zaidi wa Kifungo Kisicho na Haki

Mnamo Julai 4, 2015, Mahakama ya Wilaya ya Sabail iliongeza muda wa miezi miwili zaidi wa kuwashikilia Mashahidi wawili wa Yehova kabla kesi yao haijasikilizwa. Uamuzi huo unafanya Irina Zakharchenko na Valida Jabrayilova wasiachiliwe huru mpaka Septemba 17, 2015. Wapelelezi wanadai kwamba ni muhimu kifungo hicho ni cha muhimu wanapoendelea kujitayarisha kwa ajili ya kesi mahakamani.

Februari 17, 2015, Wizara ya Usalama wa Taifa (MNS) iliwafunga isivyo haki dada hao kwa sababu waliwahubiria majirani zao ujumbe wa Biblia. Pia, MNS bado inaendelea kuwahoji Mashahidi kuhusu kesi hiyo, wengine zaidi ya mara moja.