Vasiliy Kalin: Taarifa Kuhusu Tisho la Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova Nchini Urusi
Vasiliy Kalin, akiwakilisha Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi, anawasihi wenye mamlaka serikalini wakomeshe mateso yasiyo ya haki dhidi ya Mashahidi.
Wataalamu Wazungumzia Tisho la Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova Nchini Urusi
Wataalamu wa haki za kibinadamu wanazungumzia jinsi ambavyo kupigwa marufuku kwa Mashahidi wa Yehova kutaathiri sifa ya kimataifa ya Urusi na uhuru wa kidini wa raia wake wote.
Mahakama Kuu ya Ukrainia Yaimarisha Uhuru wa Kukusanyika kwa Amani
Mashahidi wa Yehova nchini Ukrainia sasa wanaweza kukusanyika kwenye majengo ya kukodi bila kuingiliwa.
Korea Kusini Ilimtendea Isivyo Haki Dong-hyuk Shin
Haki ya uhuru wa dhamiri na ibada wa Bw. Shin imekiukwa kwa adhabu isiyo ya haki na ya mara kwa mara kutokana na kukataa kujiunga na utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri.
Mahakama za Ujerumani Zatambua Makusanyiko ya Mashahidi wa Yehova Kuwa Sikukuu za Kidini
Sasa makusanyiko ya kila mwaka ya Mashahidi yanatambuliwa kuwa sikukuu za kidini, na kuthibitisha kwamba wazazi wana haki ya kuwaelimisha watoto kulingana na imani yao ya kidini.
Mahakama ya Ulaya Yatetea Haki ya Kidini ya Mashahidi wa Yehova Nchini Georgia
Uamuzi wa karibuni wa ECHR unalinda uhuru wa Mashahidi kukusanyika pamoja kwa ajili ya ibada na kuwaeleza majirani wao imani yao ya kidini kwa amani.
Je, Mahakama za Bulgaria Zitatetea Uhuru wa Ibada?
Mashahidi wa Yehova wamechukua hatua za kupinga uhalali wa sheria zote 44 ambazo zinakiuka haki yao ya kikatiba ya kushiriki na wengine imani yao ya dini.