Hamia kwenye habari

JUNI 8, 2018
URUSI

Wake wa Mashahidi Waliofungwa Nchini Urusi Wamtumia Mshauri wa Putin Barua Iliyo Wazi

Wake wa Mashahidi Waliofungwa Nchini Urusi Wamtumia Mshauri wa Putin Barua Iliyo Wazi

Asubuhi siku ya Juni 7, 2018, wake 10 kati ya wake 17 wa ndugu waliofungwa nchini Urusi walimtumia Mikhail Fedotov, mshauri wa Rais Putin na mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Masuala ya Raia na Haki za Kibinadamu barua iliyo wazi.