Hamia kwenye habari

JUNI 22, 2018
URUSI

Mahojiano: Dada Watano Wakumbuka Jinsi Polisi Walivyovamia Eneo la Ufa, Urusi

Mahojiano: Dada Watano Wakumbuka Jinsi Polisi Walivyovamia Eneo la Ufa, Urusi

Mapema asubuhi ya Aprili 10, 2018, wachunguzi na kikosi maalum cha polisi wakiwa wamefunika nyuso na kubeba silaha, walivamia na kupekua nyumba kadhaa za Mashahidi katika eneo la Ufa, jiji kuu la Bashkortostan, Urusi. Ndugu Anatoliy (Tolya) Vilitkevich alikamatwa, na wenye mamlaka wamemshikilia mahabusu tangu wakati huo. Dada watano kutoka Ufa, kutia ndani mke wa Tolya, anayeitwa Alyona, wanasimulia jinsi uvamizi ulivyowaathiri.