Kesi dhidi ya Dennis Christensen, iliyofanywa katika Mahakama ya Wilaya ya Oryol iliyoko Zheleznodorozhniy, imekamilika, na hakimu anatarajiwa kutoa uamuzi Jumatano, Februari 6, 2019.

Ndugu Christensen amekuwa mahabusu tangu alipokamatwa Mei 25, 2017. Kesi ya uhalifu dhidi yake ilianza kusikilizwa Februari 19, 2018. Akipatikana na hatia, mwendesha-mashtaka ameomba kwamba Ndugu Christensen afungwe gerezani kwa miaka sita na nusu.

Licha ya kufungwa kwa miezi zaidi ya 20, Ndugu Christensen amedumisha shangwe yake huku akimtegemea kabisa Yehova na akithamini sala zote zinazotolewa na ndugu ulimwenguni pote.—2 Wathesalonike 3:1, 2.