Hamia kwenye habari

Ndugu na Dada Akopyan (upande mbele katikati) na wengine waliofika kumuunga mkono mahakamani.

MACHI 6, 2019
URUSI

Mahakama Yatangua Uamuzi Dhidi ya Ndugu Akopyan Nchini Urusi

Machi 1, 2019, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Kabardino-Balkaria ilitangua uamuzi wa mahakama ya chini wa kumfunga gerezani Ndugu Arkadya Akopyan. Kesi yake imesikilizwa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Alikuwa ameshtakiwa kimakosa kwa kusambaza machapisho yenye “msimamo mkali” na “kuchochea chuki ya kidini.”

Hapo awali, mahakama ya chini ilimpa Ndugu Akopyan mwenye umri wa miaka 70 hukumu ya kufanya utumishi wa kijamii. Uamuzi huu wa karibuni wa Mahakama Kuu unatangua hukumu ya mahakama hiyo ya chini.

Tunamshukuru Yehova kwa ushindi huo na kushangilia pamoja na Ndugu Akopyan. Tunaendelea kusali kwamba ndugu zetu watavumilia kwa uaminifu.—2 Wathesalonike 1:4.