Hamia kwenye habari

Safu ya juu (kushoto hadi kulia): Ndugu Ivan Chaykovskiy na Ndugu Yuriy Chernyshev

Safu ya chini (kushoto hadi kulia): Ndugu Vitaliy Komarov, Ndugu Sergey Shatalov, na Ndugu Vardan Zakaryan

JUNI 7, 2022
URUSI

Kumtegemea Yehova Kunawasaidia Akina Ndugu Kuvumilia

Kumtegemea Yehova Kunawasaidia Akina Ndugu Kuvumilia

Mahakama ya Wilaya ya Babushkinskiy ya Moscow itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Ivan Chaykovskiy, Ndugu Yuriy Chernyshev, Ndugu Vitaliy Komarov, Ndugu Sergey Shatalov, na Ndugu Vardan Zakaryan. Mwendesha-mashtaka bado hajatuma ombi la hukumu anayopendekeza.

Mfuatano wa Matukio

 1. Novemba 24, 2020

  Maofisa wa polisi nchini Urusi walivamia nyumba 20 hivi za Mashahidi wa Yehova jijini Moscow. Maofisa hao waliwapeleka kizuizini Ivan, Yuriy, Vitaliy, na Sergey na kila mmoja akafungiwa katika chumba tofauti cha gereza. Wanahabari walikuwepo wakati nyumba ya Yuriy ilipokuwa ikipekuliwa na yeye na familia yake kuhojiwa. Baadaye habari walizokusanya zilionyeshwa kwenye vituo vya televisheni vinavyomilikiwa na Serikali

 2. Novemba 26, 2020

  Sergey aliachiliwa kutoka kizuizini na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani. Vardan, aliyekuwa amelazwa hospitalini kwa sababu ya majeraha aliyopata wakati wa uvamizi huo, alipelekwa mahabusu na kuwekwa kwenye chumba cha gereza akiwa ametengwa na wengine

 3. Novemba 27, 2020

  Mahakama iliwaachilia Ivan, Yuriy, na Vitaliy kutoka kizuizini na kuwaweka chini ya kifungo cha nyumbani

 4. Novemba 30, 2020

  Wenye mamlaka walimwachilia Vardan kutoka mahabusu na wakamweka chini ya kifungo cha nyumbani. Baada ya hayo, Vardan alituma malalamiko kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka kuhusu jinsi maofisa walivyotumia mabavu kwa njia isiyo halali walipokuwa wakifanya upekuzi

 5. Februari 16, 2022

  Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunatiwa moyo tunapoona kwamba Yehova anaendelea kuwakaribia ndugu na dada zetu wapendwa pamoja na familia zao kwa sababu wanajitahidi sana kumkaribia.​—Yakobo 4:8.