JUNI 8, 2022
URUSI
Alisaidiwa na Waabudu Wenzake
Mahakama ya Wilaya ya Vologodskiy iliyo katika Eneo la Vologda itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Yuriy Baranov na Ndugu Nikolay Stepanov. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.
Mfuatano wa Matukio
Desemba 19, 2019
Maofisa wa usalama walivamia nyumba sita za familia za Mashahidi wa Yehova katika eneo la Vologda. Ndugu Yuriy na Ndugu Nikolay walikamatwa na kuwekwa kizuizini.
Desemba 20, 2019
Ndugu Yuriy aliachiliwa na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani
Desemba 23, 2019
Ndugu Nikolay alipelekwa mahabusu
Machi 16, 2020
Ndugu Yuriy aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani, lakini hakuruhusiwa kuwasiliana na wengine ambao walishtakiwa pamoja naye katika kesi ya uhalifu, na hakuruhusiwa kutumia simu au Intaneti
Mei 19, 2020
Ndugu Yuriy aliondolewa vizuizi
Agosti 13, 2020
Ndugu Nikolay aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa katika kifungo cha nyumbani
Septemba 25, 2020
Ndugu Nikolay aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani
Machi 7, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Kuwaona akina ndugu wakiendelea kudumisha imani yao ingawa wanateswa, kunaimarisha imani sana.—1 Wathesalonike 3:7.