Hamia kwenye habari

JULAI 5, 2019
URENO

Lisbon, Ureno Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!

  • Tarehe: Juni 28-30, 2019

  • Mahali: Uwanja wa Michezo wa Lisboa e Benfica Stadium huko Lisbon, Ureno

  • Lugha ya Programu: Kiingereza, Kireno (Cha Ureno), Lugha ya Ishara ya Kireno, Kihispania

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 63,390

  • Idadi ya Waliobatizwa: 451

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,300

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Amerika ya Kati, Angola, Australasia, Brazili, Ghana, Hispania, India, Kanada, Marekani, Msumbiji, Senegal, Venezuela

  • Mambo Yaliyoonwa: Bw. Santos alikuwa mmoja wa madereva wa mabasi yaliyowabeba wajumbe. Kapteni wa basi alipomwalika kwenye kusanyiko, Bw. Santos alisema: “Ninataka kwenda. Tangu nilipoanza kufanya kazi na ningi, ninahisi amamin ambayo siwezi kuielezea. Sijui amani hii inatoka wapi, lakini mnanipatia amani. Nitakuwa uwanjani siku nzima, basi nitahudhuria.” Baada ya kuhudhuira Bw. Santos alisema kwamba alifurahia sana programu. Ametoka katika kijiji kilicho nje ya mji wa Lisbon. Alipokuwa kusanyikoni alikutana na ndugu kutoka katika kijiji kilicho jirani. Bw. Santos alipanga kukutana na ndugu huyo watakaporudi nyumbani.

 

Ndugu na dada wenyeji wakiwasalimia wajumbe waliowasili kwenye uwanja wa ndege

Wajumbe wakiwasili kwa ajili ya matembezi kwenye ofisi ya tawi nchini Ureno

Ndugu Geoffrey Jackson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho siku ya kwanza ya kusanyiko

Wahudhuriaji wakiimba kwa lugha ya ishara ya Kireno

Mmoja wa dada zetu akibatizwa

Dada kijana mwenyeji akipiga picha karibu na Kalebu na Sofia

Wajumbe wakiimba wimbo wa mwisho kwenye kusanyiko

Watumishi wa pekee wa wakati wote kutoka nchi mbalimbali wakiwapungia wahudhuriaji mwishoni mwa kusanyiko

Wajumbe wakihubiri hadharani pamoja na ndugu mwenyeji

Ndugu na dada wenyeji wakiwachezea wajumbe dansi ya kitamaduni

Ndugu na dada walioshiriki kutumbuiza kwenye tafrija ya jioni wakiwapungia mkono wahudhuriaji