Hamia kwenye habari

Jumba la Ufalme la Tortola kabla ya kufanyiwa ukarabati na baadaye. Jumba hili la Ufalme ni moja kati ya majumba matano katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Marekani yaliyoathiriwa na Kimbunga Maria na ndilo jumba la kwanza kukarabatiwa.

JANUARI 19, 2018
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Mashahidi Waharakisha Jitihada za Kutoa Msaada

NEW YORK—Jitihada za kutoa msaada zinaendelea baada ya Vimbunga Irma na Maria, ambavyo vilipiga maeneo ya Karibea na maeneo yaliyozunguka Septemba?2017. Habari zifuatazo kutoka ofisi za tawi za Barbados, Cuba, Jamhuri ya Dominika, Ufaransa, na Marekani zinaonyesha msaada ambao ndugu zetu wametoa.

Maeneo ya Ofisi ya Tawi ya Barbados—Anguilla, Antigua na Barbuda, Dominika, na St. Maarten (Upande Unaotawaliwa na Uholanzi)

Halmashauri tatu za kutoa msaada (DRCs), kutia ndani moja iliyokuwa na washiriki walioteuliwa na ofisi ya tawi ya Ufaransa, zilifanya mipango ya kupanga vikundi vya ndugu na dada wenyeji ili washughulikie mahitaji ya haraka ya wahubiri walioathiriwa na vimbunga hivyo. Kazi iliyopangwa ya kujenga upya eneo la ofisi ya tawi ya Barbados itagharimu dola milioni?2.4 na itatia ndani kurekebisha Majumba 8 ya Ufalme na nyumba 122 za ndugu zetu. Nyumba 19 zinahitaji kujengwa upya.

Jumba la Ufalme la Grand Bay, Dominika, ambalo liliharibiwa na Kimbunga Maria.

Eneo la Ofisi ya Tawi ya Kuba

Ofisi hiyo ya tawi inaripoti kwamba ndugu walioathiriwa na Kimbunga Irma wanapata msaada wanaohitaji. Hiyo inatia ndani kupata ziara za uchungaji kutoka kwa wawakilishi wa ofisi ya tawi.

Eneo la Ofisi ya Tawi ya Dominika

Halmashauri tatu zilisimamia kazi ya kutoa msaada na zilishughulikia mahitaji ya wahubiri 57 walioathiriwa. Ndugu na dada wenyeji walitoa mchango wa chakula, maji, nguo, na mahitaji mengine. Kufikia mwishoni mwa Oktoba, nyumba zote zilizoathiriwa zilisafishwa na kurekebishwa, hasa na wajitoleaji wenyeji.

Maeneo ya Ofisi ya Tawi ya Marekani—Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Marekani, Florida, Georgia, Puerto Riko, Visiwa vya Turks na Caicos

Wahubiri zaidi ya 13,000 waliathiriwa katika maeneo yaliyo chini ya ofisi hiyo ya tawi. Kwa sasa, halmashauri nne zinawasaidia ndugu na dada zetu na wamemaliza sehemu ya kwanza ya kutoa msaada, ambayo ilihusisha kusawazisha asilimia?95 ya majengo yaliyoharibiwa yanayomilikiwa na ndugu zetu na kusambaza mahitaji ya msingi kama chakula na maji. Awamu ya kwanza ya kutoa msaada bado inaendelea katika maeneo ya Puerto Riko na Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Marekani.

Mjitoleaji akisafisha nyumba ya mhubiri mmoja kati ya wahubiri 3,200 nchini Puerto Riko walioathiriwa na vimbunga hivyo.

Jumla ya wajitoleaji 690 wa ujenzi, yaani, wajitoleaji 450 kwa ajili ya visiwa na wajitoleaji 240 kwa ajili ya Florida na Georgia, watasaidia kurekebisha Majumba ya Ufalme na nyumba za ndugu zetu. Kazi inakadiriwa kugharimu dola zaidi ya milioni?30 na itahusisha mambo yafuatayo:

Maeneo ya Ofisi ya Tawi ya Marekani—Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Marekani, Florida, Georgia, Puerto Riko, Visiwa vya Turks na Caicos

Wahubiri zaidi ya 13,000 waliathiriwa katika maeneo yaliyo chini ya ofisi hiyo ya tawi. Kwa sasa, halmashauri nne zinawasaidia ndugu na dada zetu na wamemaliza sehemu ya kwanza ya kutoa msaada, ambayo ilihusisha kusawazisha asilimia?95 ya majengo yaliyoharibiwa yanayomilikiwa na ndugu zetu na kusambaza mahitaji ya msingi kama chakula na maji. Awamu ya kwanza ya kutoa msaada bado inaendelea katika maeneo ya Puerto Riko na Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Marekani.

Mjitoleaji akisafisha nyumba ya mhubiri mmoja kati ya wahubiri 3,200 nchini Puerto Riko walioathiriwa na vimbunga hivyo

Jumla ya wajitoleaji 690 wa ujenzi, yaani, wajitoleaji 450 kwa ajili ya visiwa na wajitoleaji 240 kwa ajili ya Florida na Georgia, watasaidia kurekebisha Majumba ya Ufalme na nyumba za ndugu zetu. Kazi inakadiriwa kugharimu dola zaidi ya milioni?30 na itahusisha mambo yafuatayo:

  • Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Marekani– Majumba 5 ya Ufalme, nyumba 190

  • Florida – Majumba 40 ya Ufalme, nyumba 1,174

  • Puerto Riko – Majumba 106 ya Ufalme, Majumba 2 ya Kusanyiko, nyumba 1,216

  • Turks na Caicos – Majumba 2 ya Ufalme, nyumba 56

Sala yetu ni kwamba Yehova ataimarisha mikono ya wale wote wanaosaidia kutoa msaada. Tuna uhakika kwamba kazi ya kutoa msaada, pamoja na faraja ya kiroho, itawasaidia ndugu zetu kupata nguvu tena na kuendelea kumtumikia kwa umoja Mungu wetu mkuu, Yehova.—Nehemia 2:18.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David?A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Barbados: John Medford, simu +1-246-438-0655

Jamhuri ya Dominika: Josué Féliz, simu +1-809-595-4007

Ufaransa: Guy Canonici, simu +33-2-32-25-55-55