Kimbunga Gita kiliongezeka nguvu haraka sana na kupiga maeneo ya Samoa na Samoa ya Marekani Februari 10-11, 2018, kisha eneo la Tonga Februari 12, na kusababisha mafuriko na kuharibu vitu.

Hakuna ndugu aliyeumia vibaya au aliyekufa kutokana na kimbunga hicho. Hata hivyo nyumba kadhaa zimeharibiwa sana. Halmashauri za Kutoa Msaada zimesaidia sana kuwaandalia waathiriwa mahitaji kama vile chakula na mahema.

Katika kisiwa cha SAMOA, nyumba kumi ziliharibiwa.

Nyumba tatu ziliathiriwa na maji katika SAMOA YA MAREKANI. Ndugu na dada wenyeji wamewakaribisha wale waliopoteza makao.

Nyumba sita hivi zimeharibiwa nchini TONGA. Jumba la Ufalme lilitumiwa kama makao ya muda kwa ajili ya ndugu na dada.

Tunafurahi kwamba hakuna ndugu aliyeumia sana katika janga hili na kwamba wote walioathiriwa wanapata msaada wanaohitaji kutoka kwa waabudu wenzao. Hilo linaonyesha upendo ambao Yesu alisema utakuwepo kati ya wafuasi wake.—Yohana 13:34, 35.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Samoa ya Marekani: Panapa Lui, +1-684-770-0064

Samoa: Sio Taua, +685-20629

Tonga: Palu Kanongata’a, +676-25736